Friday, July 15, 2022

Takukuru watakiwa kuwachunguza wakusanya mapato wilayani Manyoni.

 

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Singida kuwachunguza wakusanyaji wa mapato Wilayani  Manyoni kwa kuhusika na upotevu wa mapato katika standi ya mabasi Wilayani hapo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo kwenye ukumbi wa mikutano wa RC Mission Itigi alipokutana na Watumishi wa Halmashauri ya Itigi na Manyoni ambapo alibainisha kwamba kuna upotevu mkubwa wa mapato katika stendi ya mabasi kunakotokana na matumizi yasikuwa sahihi ya posi.

Amesema jumla ya mabasi yanayoingia kwenye stendi ya mabasi ni zaidi ya 200 kwa Siku na kila Basi linatozwa Tsh. 2500 lakini bado Halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya TSH. Milioni moja na laki Saba (1,700,000) kwa mwezi huku akifafanua kwamba kutokana na uchunguzi uliofanyika hivi karibuni ulibainisha bàadhi fedha kutopelekwa Benki jambo ambalo linazua sintofahamu juu yake.

Waziri Mkuu ameeleza kwamba baada ya Serikali kuona upotevu wa mapato hayo waliweka mtu mwingine ambaye katika kipindi cha wiki mbili alieleza kukusanya kiasi cha Milioni zaidi ya 20 hivyo kumtaka Kamanda wa Takukuru kuchunguza upotevu huo.

Aidha amewataka Maafisa wote ambao wanahusika katika zoezi la ukusanyaji wa mapato kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU ili kuhakikisha waliohusika wanapatikana  na fedha zinajulikana zilipokwenda.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wote wa Halmashauri hizo kuhakikisha wanasimamia miradi iliyopo ili iweze kuwanufaisha wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kikao cha ndani cha kuzungumza na watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa RC Mission Itigi.

No comments:

Post a Comment