Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko leo Desemba 4,
2021 amefungua rasmi maadhimisho ya miaka
60 ya Uhuru Tanzania Bara yaliyofanyika ki Mkoa wilayani Manyoni mkoani Singida
katika uwanja wa Jumbe ambapo Watumishi mbalimbali walishirikishwa.
Akihutubia mamia ya Watumishi kutoka wilaya ya Ikungi,
Manyoni, Iramba, Singida mjini, Mkalama na Itigi amewashukuru Watumishi hao kwa
nidhamu kubwa walionesha wakati wa bonanza la michezo lililofanyika katika
uwanja huo na kushirikisha michezo ya kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume, netiboli,
mpira wa miguu, kukimbiza kuku, mcho wa bao, riadha na mashindano ya kula.
Hata hivyo RAS Mwaluko akatumia muda huo kuzipongeza timu mbalimbali
zilizoshinda katika bonanza hilo pamoja na watumishi walioshiriki katika
michezo na mazoezi mbalimbali ambapo akawaasa kuendelea kufanya mazoezi hata
baada ya bonanza kwisha ili kulinda afya zao.
RAS Singida akawataka
watumishi hao kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru kwa kujitathimini walipotoka walipo na wanapokwenda ili kuona
maendeleo ambayo nchi yetu imeweza kuyafikia katika kipindi hicho.
Dorothy Mwaluko akaenedelea kufafanua kwamba Mkoa wa Singida
unafursa nyingi ikiwemo za kitalii ambazo zikitumika vizuri zitaongeza vipato vya wananchi na kuboresha maisha yao.
Aidha akawataka watumishi hao kuadhimisha miaka 60 kwa kujitathmini
namna wanavyoutumia muda wao kwa kutambua kwamba ni mtaji ambao kama
hautatumika vizuri mafanikio hayataweza kufikiwa.
Kwa upande wake Henry Kapera
Afisa michezo wa Mkoa wa Singida akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni RAS
Singida amesema lengo la michezo hiyo ni
kuadhimisha miaka 60 ya uhuru na
kuwajenga watumishi ki afya.
Hata hivyo Kapera akawaomba wananchi wa Mkoa huo wanawake na
wanaume kujitokeza na kushiriki michezo
mbalimbali inayoendelea uwanjani hapo kama sehemu ya mazoezi lakini kuonesha
vipaji vyao.
Aidha Kapera alibainisha kwamba baadhi ya timu zilichelewa
kufika uwanjani hapo kutokana na sababu mbalimbali hivyo wangeweza kuendelea na
michezo mbalimbali baada ya mgeni rasmi kuondoka.
Kapera akamalizia kwa kusema mkoa una mkakati kabambe kuendeleza michezo hiyo pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA BONANZA
No comments:
Post a Comment