Wakazi wa
Mkoa wa Singida wametakiwa kujenga tabia ya kuyatembelea maeneo ya historia na
kijifunza histrioa ya mkoa wao na nchi yao kwa ujumla ili waweze kutambua
walivyokuwa wakiishi watu wa maeneo hayo kabala na baada ya uhuru.
Imebainika
kwamba ili kujua hatua ambazo nchi imeweza kupiga na kuleta maendeleo ya
uchumi, siasa na utamaduni ni lazima kuijua historia ya zamani ikilinganishwa
na hali ilivyo kwa sasa.
Hayo
yamesemwa leo Desemba 5, 2021 na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko
wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya kihistoria yakiwemo Ofisi ya DC wa
kwanza Muafrika iliyopo Manyoni Mkoani Singida, Nyumba aliyolala Mwalimu
Nyerere iliyopo eneo la Mjini Kati Manyoni, vituo mbalimbli vya kihistoria eneo
la Kilimatinde na reli ya mwendo kasi iliyopo Makutopora ambapo alibanisha
umuhimu wa kujifunza historia ya maeneo hayo.
Ziara hiyo
ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru ambayo Mkoa wa Singida
unaendelea kuadhimisha kwa namna tofauti mpaka itakapofika Desemba 8 mwaka huu
kabla ya kuungana na maadhimisho ya ki taifa yatakayofanyika tarehe 9 katika
uwanja wa uhuru mkoani Dar es salaam.
Mwaluko
akafafanua kwamba pamoja na historia lakini wananchi wa Mkoa wa Singida
wanapashwa kufahamu jitihada za Serikali katika kuliletea taifa maendeleo kwa
kuanzisha reli ya mwendo kasi ambayo imesemekana itarahisisha usafiri na
kuongeza biashara maeneo mbalimbali.
Ziara hiyo
ilihusisha wakurungezi wa Halmashauri saba za Mkoa wa Singida, Wakuu wa Wilaya
ya Singida Mjini na Iramba pamoja na wabunge mbalimbali lengo likiwa ni
kuwaonesha wananchi fursa nyingine za ki utalii ambazo huweza kulisaidia taifa
kupata mapato kupitia vitu vya kihistoria.
Naye DC wa
Singida Mjini Mhandisi Pasikas Muragili akimwakilisha DC wa Manyoni akatumia
muda huo kuwataka Vijana kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kuwa
yana mafunzo ndani yake.
DC Muragili
akawataka pia vijina kujitokeza siku ya tarehe sita katika ukumbi wa mikutano
wa Halamashauri ya wialaya ya Manyoni kushiriki kongamano juu ya hatua mbalimbali
zilizofikiwa na Serikali kabala na baadaye.
No comments:
Post a Comment