Monday, December 06, 2021

Maadhisho ya miaka 60 ya Uhuru mkoani Singida vijana wafanya Kongamano

 

Vijana wametakiwa kuenzi miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara na miaka 59 ya Jamhuri kwa kuangalia  mabadiliko katika nyanja za uchumi utamaduni na namna ya upatikanaji wa viongozi unavyofanyika hapa nchini.

Akiongea katika kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,  Mkuu wa ya Iramba Suleimani Mwenda amesema hali ya uchumi wa taifa umebadilika kwa kiasi kikubwa kabla na baada ya uhuru hivyo vijana wanatakiwa kujifunza kutokana na mabadiliko hayo.

DC  Suleimani akabainisha kwamba katika kipindi cha baada ya uhuru kulikuwa na chuo Kikuu kimoja  cha Dar es Salaam ambacho kilichukua wanafunzi wachache hivyo kusababisha waliowengi kukosa fursa ya kupata elimu ya juu, ikilinganishwa na kipindi hiki ambapo vyuo ni vingi.

Amesema ukizungumzia uhuru wa Tanzania unazungumzia uhuru wa nchi nyingi za kiafrika kwakuwa Tanzania ilishiriki katika kutafuta ukombozi wa mataifa mengi ya kiafrika  yakiwemo  Msumbiji, Afrika ya Kusini jambo ambalo vijana wanatakiwa kufahamu hali ya ukarimu ambao umekuwa ni sehemu ya utamaduni wetu. 

Aidha siasa za Tanzania hasa namna ambavyo viongozi wamekuwa wakibadilishwa kwa njia ya chaguzi ambapo mataifa mengi yamekuwa yakishikwa na butwaa hasa kwa kuangalia nchi za jirani na Tanzania ambazo zimekuwa zikiingia kwenye migongano mara kwa mara.

Awali DC huyo alitoa shukrani za dhati kwa wandaaji wa kongamano hilo ambalo linawafungua vijana na kuwafanya kuwa wazalendo na kuwaonesha fursa mbalimbali zinazowazunguka.

DC Mwenda akabainisha umuhimu wa kufanyika kongamano hilo wilayani Manyoni kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya  kuwafundisha vijana umuhimu wa Mashujaa waliotokea Manyoni katika mapambano ya kudai uhuru.

Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida Fredrick Ndahani akaishukuru Serikali kwa kufufua na kuendeleza shirika la ndege nchini na ambapo  awali lilikuwa na ndege moja  lakini  baada ya miak 60 ya uhuru shirika lina ndege 11.

Ndahani alisema shirika hilo linatoa fursa kwa vijana kufanya biashara ndani na nje ya nchi kwa kwa kuwa miundombinu ya barabara  na anga vimeendelezwa kwa kiasi kizuri.

Bwana Ndahani akafafanua kwamba ni jukumu la vijana kulinda miundombinu ya barabara na reli kwa kuwa ndio vitu ambavyo vitawakomboa vijina katika mpango wa usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.

Afisa Vijana huyo akamalizia kwa kusema kwamba mkoa wa Singida unajivunia kuwa na shule nyingi za Sekondari na Msingi ambapo hakuna kijana ambaye ataweza kufaulu akakosa shule alifafanua Ndahani.

Kongamano hilo lilihusisha vijana wajasiriamali, wanafunzi wa shule mbalimbali za wilayani hapo, Maafisa wa Serikali pamoja na umoja wa vijana wa chama cha Mapindizi CCM.

Mkuu wa ya Iramba Suleimani Mwenda akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo (kushoto kwake) Afisa Vijana Mkoa wa Singida Fredrick Ndahani  

Elimu ya Afya ikitolewa

Mwanafunzi akijibu swali wakati wa kongamano hilo







picha za pamoja

No comments:

Post a Comment