Kipindi cha miaka 60 ya uhuru Mkoa wa Singida umejitosheleza kwa chakula
na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya biashara yakiwemo Alizeti, ufuta, dengu, korosho na vitunguu
kutokana na mabadiliko katika matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye kilimo.
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge wakati
wa kilele cha maadhimisho ya kimkoa ya miaka 60 ya uhuru yalifanyika katika
uwanja wa Jumbe wilayani Manyoni mkoani hapo.
Uzalishaji wa mazao makuu ya chakula umeongezeka kutoka Tani 197,886
mwaka 1990 hadi kufikia Tani 821,882 mwaka 2020/2021.
“uzalishaji wa mazao ya chakula ya kipaumbele ambayo ni mtama, uwele,
viazi vitamu na muhogo, uzalishaji wa mazao haya uliongezeka kutoka Tani
194,878 mwaka 2005/2006 hadi kufikia Tani 395,594 mwaka 2020/2021” Amesema Dkt.
Mahenge.
Aidha amebainisha kwamba uzalishaji wa mazao ya biashara ya kipaumbele
ambayo ni alizeti, pamba, vitunguu, na korosho uliongezeka kutoka Tani 41,746
mwaka 2005/2006 hadi Tani 230,793 mwaka 2020/2021. Zao la alizeti pekee uzalishaji umeongezeka
kutoka Tani 28,917 mwaka 2005/2006 hadi Tani 222,8000 mwaka 2020/2021,
aliendelea kufafanua RC Mahenge.
Wakati wa Utawala wa Mkoloni Singida hapakuwa na kiwanda kikubwa na vya
kati hata kimoja wakati wa Uhuru na sasa vipo 9 mwaka 2020/2021.
Akizungumizi ongezeko la viwanda katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru RC
Mahenge amebainisha kwamba Mwaka 1961 hapakuwa na viwanda vya usindikaji wa
alizeti lakini mwaka 2021 kuna jumla ya viwanda 204 vinavyofanya kazi.
“Mwaka 1961 viwanda vidogo vilikuwa ni vichache na vilikuwa vya fani ya useremala, uhunzi na utengenezaji chumvi,
na sasa vipo jumla ya viwanda vidogo 1,309 vinavyofanya shughuli mbalimbali
mwaka 2020/2021” alieleza RC Mahenge.
Akieleza kuhusu huduma ya afya amefafanua kwamba Mkoa kwa sasa una jumla
ya vituo vya kutolea huduma za Afya 246 ambapo Hospitali kumi na moja (11),
vituo vya Afya 20 na Zahanati 211.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa akaeleza kwamba mkoa umepokea fedha za tozo Sh. Bilion 2.2 kwa
ajili ya vituo vya Afya tisa (9) na kupitia Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa
Taifa na mapambano ya UVIKO 19 Sh.Bilion 1.94 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi
wa majengo ya dharula katika Hospitali za wilaya, wagonjwa mahututi na nyumba
za watumishi.
MATUKIO KATIKA PICHA
No comments:
Post a Comment