Tuesday, June 20, 2023

Kilimo cha Umwagiliaji Mkoani Singida kuwatoa vijana Kimasomaso.

Halmashauri za Wilaya Mkoani Singida zimetakiwa kutafuta maeneo yenye ukubwa wa ekari zisizopungua 500 ambazo zitajengewa miundombinu ya umwagiliaji na kugawiwa kwa vijana wa kiume na wakike wapatao 100.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba,  alipotembelea Halmashauri ya Singida na Ikungi ameeleza nia yake ya kuwasaidia vijana wa Mkoa huo kwa kuanzisha mashamba ambayo yatawasaidia kuongeza vipato kwao na Halmashauri.

Amesema kwamba mashamba hayo yatakuwa ni kwa ajili ya Kilimo cha mahindi na vitunguu ambapo Halmashauri zitawalimia na kuwapatia mikopo huku Wizara ya Kilimo ikiwa imeahidi kwamba watachimba visima vya umwagiliaji ambavyo vitatumia mabomba.

Hata hivyo amebainisha kwamba mikopo hiyo itakayotolewa na Halmashauri kwa vijana watarejesha baada ya miaka mitatu ikiwa ni mbegu, huduma ya kusafisha mashamba na uwekaji wa miundombinu.

Kwa upande wake DC wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili amempongeza RC kwa kuja na wazo hilo kwakuwa kwanza utaongeza vipato kwa vijana hasa kipindi hiki ambacho kilimo ndicho kinacho ongoza kwa kuleta mapato kwa Serikali.

Amesema  kwa sasa wanachangamoto ya wataalamu wa upimaji wa ardhi ambao watasaidia kupima maeneo yanayomilikiwa na Halmashauri hiyo ikiwemo shule vituo vya Afya na maeneo mengine.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elia Digha, amesema wamejipanga kuongeza mapato kwa kuongeza vyanzo vipya vikiwemo kuboresha na kukodisha majengo yao na uuzaji wa viwanja.

Aidha Digha amemuomba Mkuu wa Mkoa kusaidia upatikanaji wa miradi katika Wilaya hiyo ili kuepuka kutegemea kilimo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akizungumza na Madiwani wa halmashauri hiyo wakati akifungua kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Ikungi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani lililofanya katika ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari Ilongero Wilayani Singida vijijini.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson, akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Wilayani Ikungi Juni 20, 2023.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini wakati wa kikao kilichofanyika katika shule ya Sekondari Ilongero.


No comments:

Post a Comment