Monday, May 01, 2023

Serukamba aagiza TAKUKURU kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi kukomesha rushwa ya ngono.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba leo ameiagiza Taasisi ya kudhibiti na kupambana na rushwa ((TAKUKURU) Mkoani hapo kushirikiana na vyama vya wafanyakazi kutokomeza rushwa katika maeneo ya kazi ikiwemo rushwa ya ngono ambayo imeonekana kushamiri sehemu nyingi.

Maagizo hayo ameyatoa leo wakati wa sherehe za wafanyakazi Mei mosi iliyofanyka ki Mkoa katika uwanja wa Liti uliopo Manispaa ya Singida ambapo alieleza changamoto ya rushwa inavyoweza kurudisha maendeleo nyuma ya Mkoa huo.

Aidha Serukamba ametoa muda wa kipindi cha miezi mitatu Taasisi hiyo imletee taarifa ambavyo wametengeneza mikakati ya kupambana na aina hizo za rushwa.

" Kumekuwepo na tatizo la rushwa ya ngono katika maeneo yetu ya kazi naelekea  TAKUKURU kwa kushirikiana na Vyama vya wafanyakazi kukomesha swala hilo na natoa muda wa miezi mitatu nipate taarifa namna ambavyo umeweza kulidhibiti" alisema Serukamba.

Kwa upande wake Mratibu  wa TUCTA Mkoa wa Singida, Maria John Bange ameiomba Serikali  kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao za kisheria  na mafao ya kustaafu kwa wakati, jambo ambalo mgeni rasmi RC Serukamba alilitolea maelekezo kwa Wakurugenzi kuhakikisha wanalipa stahiki hizo huku akitoa maelekezo kwa Shirika la Bima na NSSF kuhakisha wanawalipa mafao kwa wakati.

Hata hivyo  Mratibu huyo  ameomba Serikali kuhakikisha mabaraza ya wafanyakazi yanafanyika kwa wakati na uwepo wa staha katika sehemu za kazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida akizungumza na wafanyakazi wa mkoa wa Singida katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Liti Singida Mjini.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA














No comments:

Post a Comment