Friday, April 14, 2023

Mashamba ya Shule kutumika kuzalisha chakula cha wanafunzi - Dr. Mganga.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga ameagiza  mashamba yote ya shule katika msimu ujao wa kilimo yatumike kuzalisha mazao ya Kilimo na biashara kwa kiasi kikubwa ili wanafunzi  wapate chakula cha kutosha ambapo amesema itasaidia kuongeza ufaulu.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 14.04.2023 katika Mkutano wa ALAT unaoendelea kwa siku ya pili katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo RAS huyo ameeleza nia yake ya kuondoa utoro kwa wanafunzi na kuongeza ufaulu huku akieleza kwamba kilimo kwa wanafunzi kitaongeza upatikanaji wa chakula shuleni.

Aidha RAS Fatma ameendelea kueleza kwamba shule nyingi za Mkoa wa Singida zina maeneo makubwa yanayofaa kilimo lakini yanatumika kuzalisha kiasi kidogo sana jambo ambalo linaongeza mzigo mkubwa kwa wazazi katika zoezi la kuchangia chakula shuleni.

"Serikali imeleta madarasa iliyobaki ni sisi viongozi kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria darasani, wazazi kuhakikisha wanawalisha wanafunzi, lakini litakuwa jambo jema watoto wetu wakaanza kuyatumia mashamba ya shule kuzalisha chakula chao wenyewe" Dkt. Fatma Mganga.

Aidha, RAS amewaagiza Maafisa elimu wote mkoania hapo kuhakikisha wanatumia mbinu mbalimbali za kufundishia zikiwemo matumizi ya vijiti vya kuhesabia ili kuondoa tatizo la baadhi ya wanafunzi kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu huku akiitaja shule ya msingi Kisasida iliyopo Manispaa ya Singida yenye wanafunzi zaidi ya 1000 kati ya hawo 139 hawajui kusoma na kuandika.

Hata hivyo amewataka walimu kuwa na nia ya dhati katika kuondoa tatizo la KKK shuleni kwani wazazi wanawategemea katika mabadiliko ya watowa wao.

RAS ameeleza amewasihi Wakurugenzi na wenyeviti wa Halmashauri kuhakikisha wanatumia sheria ndogo kuondoa tatizo la utoro shuleni ili kuinua viwango vya elimu.

MATUKIO KATIKA PICHA













 

No comments:

Post a Comment