Thursday, April 13, 2023

Eneo la kilimo cha alizeti mwakani kufikia ekari Milioni moja Mkoani Singida - Serukamba

Mkoa wa Singida umejipanga kuongeza eneo la uzalishaji wa Alizeti kutoka ekari 631,931 mpaka kufikia ekari Milioni moja (1,000,000) kwa kutumia wakulima wadogo wakati, wakubwa na vikundi ili kuongeza uzalishaji wa Mafuta ya alizeti.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba wakati akihutubia katika mkutano wa ALAT uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Ikungi na kuhusisha wenyeviti wa Halmashauri Sita, Madiwani wawili kwa kila Halmashauri na Wakurugenzi.

Amesema zao la Alizeti ndio kitambulisho cha Mkoa huo hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha eneo la kilimo linaongezeka ambapo RC amebainisha kwamba ushirikiano wa viongozi wa vijiji na kata pamoja na Maafisa kilimo kuhakikisha wanahamasha wakulima kuongeza maeneo na vijana kuwekeza katika Kilimo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisita jambo wakati wa mkutano huo.

Aidha amefafanua kwamba ukuaji kwa kasi jiji la Dodoma kunatoa fursa kwa Mkoa wa Singida kuzalisha mazao ya chakula na mafuta kwa kasi huku akibainisha kwamba ufunguliwaji wa barabara za Singida Mbeya, Singida, Arusha, Singida, Tanga litaongeza soko na ukuaji mkubwa wa Mkoa huo.

RC Serukamba amefafanua kwamba mpaka kufikia msimu wa kilimo wa mwaka kesho Singida kutakuwa na wakulima wa aina Tatu ambao ni wakulima wadogo, wa Kati na wakubwa watakaolima zao la alizeti ili kukidhi haja ya soko ambalo mpaka sasa bado halijatengemaa.

Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justuce Kijazi kwa kutenga eneo lenye ukubwa wa ekari elfu 50 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kilimo cha pamoja unaotekelezwa na Wizara ya Klimo kwa vijana "build better Tomorow" ambapo RC Serukamba amesema taratibu za kufanya uchambuzi wa kina utaanza ili kujenga Miundombinu ya Umwagiliaji.

Akimalizia hotuba yake amewaagiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanatumia fedha walizopewa kwa manufaha kabla ya tarehe 30 Juni na kuhakikisha  hakuna fedha inayobaki.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, wakati wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa ALAT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Jamse Mkwega akizungumza wakati wa mkutano huo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akizungumza wakati wa mkutano huo.













No comments:

Post a Comment