Tuesday, April 11, 2023

Halmashauri zatakiwa kusimamia matumizi ya fedha za miradi na kuhakikisha zinatumika kabla ya mwisho wa bajeti.

Halmashauri za  Mkoani Singida zimetakiwa kuongeza umahiri katika usimamizi wa miradi mbalimbali  ikiwemo mradi Boost ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa gharama zilizokusudiwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha kumalizika.

Maelezo hayo yametolewa leo tarehe 11/04/2023  na Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa elimu, Wahandisi na Maafisa manunuzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo.

RC Serukamba ameelekeza viongozi kusimamia na kutembelea miradi mara kwa mara ili kutatua changamoto ambazo zinaweza kuibuka wakati wa utekelezaji huku akiwataka Wakuu wa Wilaya wote kukutana na wauza saruji ili kukubaliana gharama za ununuzi na ufikishwaji wa saruji katika maeneo ya kazi.

Hata hivyo amewataka Wakurugenzi kuwalipa kwa awamu mafundi watakaotekeleza ujenzi wa madarasa hayo huku akitoa tahadhari kwa mafundi ambao wamekuwa na tabia ya kutowalipa vibarua waliofanya nao kazi na kusababisha kazi kuchelewa.

Aidha Wakurugenzi walimueleza RC Serukamba kwamba tayari washapata maeneo kwa ajili ya ujenzi na kamati za ujenzi zimeshaundwa hivyo kazi ya ujenzi itaanza muda wowote hivyo kumlazi RC kutoa maelekezo mengine kwa Wakurugenzi na taasisi zinazohusika na upimaji wa aridhi kuhakikisha maeneo hayo yanapimwa na wanapata hati miliki katika kipindi kifupi.

Akimalizia maagizo yake Serukamba amesema kila Mkuu wa Idara apewe sehemu ya kusimamia katika ujenzi huo huku akiwataka wahandisi kuongeza usimazi na kuhakisha kabla ya mwezi ya sita kazi hiyo inakamilika.

Awali akifungua kikao hicho Serukamba alibainisha kwamba  Mkoa wa Singida umepokea jumla ya Tsh. Bilioni 9.024 kutoka Mradi wa boost unashugulikia uboreshaji wa elimu.

Amesema fedha hizo ni maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo madarasa matundu ya  choo pamoja na madawati imegawanywa kama ifuatavyo,  Ikungi wamepata Bilioni 1.47 Iramba bilioni 1.59 Itigi 1.39 Manyoni Milioni 909 Mkalama Milioni 925 Singida DC Bilioni 1.351 na Manispaa wamepata Bilioni 1.371 alisema

Mwisho


 

No comments:

Post a Comment