Tuesday, November 29, 2022

Serukamba Awaita Wawekezaji Kuwekeza Singida

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, amewataka Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza Mkoani Singida kwa kuwa kuna uwepo wa miundombinu bora ya barabara za kufika mikoa yote nchini, hoteli na nyumba mbalimbali kwa ajilia ya mikutano huku akieleza ukarimu wa watu wa Mkoa huo.


Kauli hiyo ameitoa leo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika Kitaifa katika uwanja wa stendi ya zamani uliyopo Singida Mjini ambapo ameeleza kwamba Mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji katika Kilimo, viwanda na uendeshaji wa mikutano mbalimbali.

Aidha ameeleza kwamba Mkoa wa Singida unatekeleza mipango yake kwa kupitia Takwimu za Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambapo Mkoa una watu wapatao 2,008,058 ambapo Wanawake ni 1,012,355 na Wanaume ni 995,703

Aidha amepongeza Shirika la Taifa la Takwimu (NBS) kwa maamuzi yao ya kufanya mkutano huo Mkoani Singida ambao umesaidia kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi wa hapo.

Mkutano huo ulianza tarehe 28/11/2022 katika ukumbi wa mikutano KBH ambapo kulikuwa na Kongamano na kuhudhuriwa na wadau zaidi ya Mia mbili.


Naibu Waziri Kilimo Anthony Peter Mavunde (Mb), (Mgeni rasmi) akihutubia wananchi waliohudhuria kwenye Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika tarehe 29 Novemba, 2022 katika uwanja wa stendi ya zamani Mjini Singida

Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Anne Semamba Makinda, akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani Mjini Singida 29 Novemba, 2022 

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani Mjini Singida 29 Novemba, 2022 









Matukio mbalimbali yakiendelea wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani Mjini Singida 29 Novemba, 2022 

Kikundi cha ngoma za Asili kutoka Mkoani Singida kikitoa burudani

No comments:

Post a Comment