Tuesday, September 13, 2022

Wananchi wa Kihanju wakabidhiwa Mradi wa maji wenye thamani Milioni 293

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mapokezi ya mradi wa kisima cha maji kwa wananchi wa kijiji cha Kihanju halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni.

Wananchi zaidi ya 2,000 wa Kijiji cha Kihanju Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni wameishukuru Serikali na Shirika la Water Aid kwa kuwajengea kisima cha kisasa cha maji ambacho kitasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji na kuimarisha shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo.

Akihutubia wananchi wa Kijiji hicho leo baada ya uzinduzi na makabidhiano ya mradi huo kwa jumuiya za watumia maji za Kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wananchi hao kushiri katika shughuli za uendeshaji na matengenezo ya kisima hicho kwa kushirikiana na kamati za maji za  Kijiji hicho zilizoundwa ki sheria.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akihutubia baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji.

Hata hivyo RC Serukamba amewakumbusha wananchi hao kulipia huduma za maji kwa wakati huku wakitakiwa kutunza vyanzo vya maji na kulinda miundombinu isiweze kuharibika ili waendelee kunufaika na Mradi wa maji safi kwa muda mrefu.

Aidha Serukamba amezitaka jumuia za maji kupanga bei za maji kulingana  na gharama za uzalishaji wa maji hayo pamoja na kupanga mipango ya muda mrefu na mfupi ambayo itasaidia kurejesha gharama za uendeshaji na matengenezo huku akikumbusha  kuangalia uwezekano wa kulifikia kundi la watu wasiojiweza  ili waweze kupatiwa maji.

Hata hivyo RC Serukamba ameagiza wananchi wa Kijiji cha Kihanju kutumia uwepo wa maji hayo kujiongezea kipato kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa kuwa wanatumia muda mfupi kupata huduma ya maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vinywaji la Serengeti SBL Mark Ocitti amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Milioni 293.19 na utahudumia wakazi zaidi ya 2000 na kuendeleza shughuli za kijamii ikiwemo ujenzi wa hospitali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la vinywaji la Serengeti SBL Mark Ocitti akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi kisima.

Amesema kwamba Sekta ya kilimo katika maeneo hayo inategemewa kukuwa kwa kiasi kikubwa kwakuwa kutakuwa na maji lakini pia uwepo wa muda wa kutosha ambapo mashirika mbalimbali yatafanya uwekezaji kuongezeka.

Amesema kupitia programu za kijamii 2030 wametoa kipaumbele katika utoaji wa ujuzi wa maisha kupita ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosomea kilimo katika programu ijulikanayo kama Kilimo viwanda ambayo imefadhili wanafunzi 200 tangu mwaka 2019.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amebainisha kwamba Kisima hicho kitakuza shughuli za kiuchumi za kilimo ambazo zitachochea wataalamu wakubwa wa Biashara ya Kilimo ambao watatoa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu za shayiri, mtama na mahindi ambapo Shirika hilo limekuwa likinunu zaidi ya Tani 18,000 kwa mwaka kutoka kwa wakulima.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wilaya ya Manyoni Mhandis Gabriel Ngongi amesema katika bajeti ya mwaka huu Mamlaka imetenga jumla ya TSH Milioni 30 kwa ajilia ya kupelea maji katika vijiji vingine vitatu kutokea Mradi ulipo.

Aidha ameushukuru ushirikiano uliofanywa na Shirika la water Aid na Serengeti Breweries kwa mchango wao wa Kisima chenye uwezo wa Lita 7000 na pampu yenye uwezo mkubwa.

Awali akitoa Tathmini Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said amesema mtandao wa maji mjini umefikia asilimia 78 wakati mtandao wa maji Vijijini umefikia asilimia 61.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA






















No comments:

Post a Comment