Thursday, November 10, 2022

RAS Singida aomba wadau wa Maendeleo kutia nguvu uboreshaji wa lishe

 

Wadau wa Maendeleo Mkoa wa Singida wameombwa kusaidia upatikanaji na uboreshaji wa Lishe mashuleni ili kuondoa changamoto ya utapiamlo kwa watoto wa chini ya miaka mitano pamoja wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Ombi hilo limetolewa leo tarehe 10.11.2022  na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko alipokutana na Kamati ya Lishe ya Mkoa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkoa huo.

 Amesema kwa sasa Mkoa unatekeleza afua mbalimbali za Lishe na inaendelea kutoa mafunzo ya Lishe na mapishi katika Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya  na chakula mashuleni.

"Lishe ni  mtambuka  ambapo kila mtu anatakiwa kulitekeza kwa upande wake, tukitegemea fedha za Serikali peke yake tutachelewa, naomba wadau mbalimbali wasaidie kuongeza virutubishi kwenye vyakula mafuta ya kula unga wa uji na chumvi" alisema Mwaluko.

Aidha amewaagiza Maafisa Lishe Mkoani hapo kutembelea vituo vya Lishe pamoja na utoaji wa elimu kwa kina mama wajawazito na wananchi kwa ujumla.

 Afisa Lishe Mkoa wa Singida Cristowela amesema Halmashauri zote zilifanya maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kwa kutoa elimu ngazi ya kituo na jamii ambapo jumla ya wazazi na walezi 18,843 walipata elimu ya unyonyeshaji.

Aidha Cristowela amesema jumla ya vijiji  362 kati ya 441 sawa na asilimia 82 mitaa 23 kati ya 53 sawa na asilimia 43 waliadhimisha siku ya Afya na Lishe  na utoaji wa elimu ya lishe kwa makundi mbalimbali katika jamii.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA 


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Lishe wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment