Tuesday, July 14, 2015

DOKTA KONE AZINDUA KITUO CHA POLISI MANG'ONYI WILAYANI IKUNGI NA MIRADI MINGINE ILIYOJENGWA KWA UFADHILI WA MGODI WA SHANTA.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akisoma maandishi mara baada ya kukizindua rasmi kituo cha polisi cha Mang'onyi Wilayani Ikungi. Pembeni yake ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mgodi wa SHANTA Roman Urassa.
  
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akifungua geti la kuingia katika kituo cha polisi cha Mang'onyi Wilayani Ikungi. 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akizungumza na askari polisi ndani ya kituo cha polisi cha Mang'onyi Wilayani Ikungi. Pembeni yake ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka na  nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Charles Gishuli.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akifungua bomba la maji katika kijiji cha Mang'onyi Wilayani Ikungi ikiwa ni moja ya miradi iliyojengwa kwa ufadhili wa Mgodi wa SHANTA.
 
Anna Peter Kweka Mkazi wa Kijiji cha Mang'onyi Wilayani Ikungi akisaidiwa kubeba ndoo ya maji na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone mara baada ya kuzindua mradi wa maji Kijijini hapo.


Anna Peter Kweka Mkazi wa Kijiji cha Mang'onyi Wilayani Ikungi akibeba ndoo ya maji kutoka katika bomba la maji lililojengwa kijijini hapo kwa ufadhili wa Mgodi wa SHANTA na Kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akizindua kwa kukata utepe chumba cha mashine ya kusukuma maji katika chanzo cha maji kijijini Mang'oni Wilaya ya Ikungi.
  
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko V. Kone akizindua kwa kukata utepe darasa moja katika shule ya Msingi Mlumbi lililojengwa na Mgodi wa SHANTA Wilaya ya Ikungi.

No comments:

Post a Comment