Wednesday, January 07, 2015

MGANGA MKUU MKOA WA SINGIDA DOKTA DOROTHY GWAJIMA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WIZARA YA AFYA.
















Aliyekuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Dorothy Gwajima na  sasa Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

"Viongozi wa Afya mnatakiwa kuhakikisha watumishi wote waliopo ndani ya taasisi yenu wanaheshimiwa na kupewa stahiki zao pasipo ubaguzi unaotokana na tofauti zao za taaluma, elimu au mambo mengine".
Nasaha hizo zimetolewa na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Dorothy Gwajima alipokuwa akiwaaga watumishi wote wa sekta ya Afya na Ustawi wa jamii na waandishi wa habari Mkoani Singida ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Dokta Gwajima amesema katika utumishi wake Mkoani Singida kwa muda wa miaka minane ameshirikiana na watumishi wengine kufanikisha kuimarika kwa Mfuko wa Afya ya jamii hadi kufikia asilimia 47 na kuongezeka kwa mapato ya uchangiaji hospitali kwa mfuko wa bima ya afya kutoka milioni 7 hadi milioni 30 kwa mwezi. 
Amewaasa watumishi wa afya Mkoani Singida kutambua kuwa inawezekana kufanya kitu chema  ndani ya rasilimali chache zilizopo na kuinua ubora wa huduma za afya kwa wananchi.

















Afisa Utumishi Mkoa wa Singida Bw. Samson Thomas Ntunga.
Kwa upande wake Afisa Utumishi Mkoa wa Singida Bw. Samson Thomas Ntunga amemshukuru Dokta Gwajima kwa usimamizi mzuri wa sekta ya afya na ustawi wa jamii Mkoani Singida na mafanikio aliyoyapata.
Ntunga amesema Dokta Gwajima amekuwa mtumishi chapakazi na mwadilifu kama sifa ya watumishi wa Mkoa wa Singida ilivyo hadi mchango wake kutambulika kitaifa na kupewa majukumu makubwa ya kitaifa.
Amesema watumishi waliobaki wanapaswa kuendeleza juhudi za Dokta Gwajima na kuwa wabunifu zaidi ili sifa nzuri na mafanikio makubwa ya Hospitali ya Mkoa wa Singida yaongezeke.

















Watumisi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakiwa katika kikao cha kumuaga aliyekuwa Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Dokta Dorothy Gwajima.

















Watumisi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa Mganga Mkuu Mkoa wa Singida Dokta Dorothy Gwajima.

No comments:

Post a Comment