Tuesday, March 18, 2014

UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOANI SINGIDA MACHI 16-22, 2014


Maadhimisho ya wiki ya maji mjini Singida yamezinduliwa rasmi leo Machi 17, 2014 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Vicent Parseko Kone katika eneo la Mantanki ya Maji Mandewa huku akisisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.

Dk Kone amesema Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Singida (SUWASA) inapaswa kuhakikisha wananchi wa Singida wanapata maji safi na salama. Kauli mbiu ya maaadhimishoya wiki ya maji kwa mwaka 2014 ni "Maji na Nishati".


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akimsalimia Injinia wa Maji Mkoani Singida Yunus Rugeiyamu mara baada ya kuwasili katika  eneo la matanki ya maji Mandewa katika maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Singida.


Watumishi wa serikali na wananchi waliofika katika  eneo la matanki ya maji Mandewa katika maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Singida.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akipanda mti wa mchungwa katika  eneo la matanki ya maji Mandewa katika maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwl Queen Mlozi akipanada mti katika  eneo la matanki ya maji Mandewa katika maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Singida.

 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akipanda mti katika eneo la matanki ya maji Mandewa katika maadhimisho ya wiki ya maji Mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment