Wednesday, March 12, 2014

HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA 59 LIANA HASSAN KATIBU TAWALA MKOA WA SINGIDA.


Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan akilishwa keki na mfanyakazi mwenye umri mdogo kuliko wote ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Faraja Alfayo Kataze Mhasibu Msaidizi, katika ukumbi wa mikutano ofisini hapo leo asubuhi, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Vincent Parseko Kone.


Zawadi ya keki iliyotolewa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.

Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida wakimuimbia wimbo maalum wa siku ya kuzaliwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw Liana Hassan leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano ofisini hapo.

Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Singida Bw Fidelis Mdala akimpa mkono wa heri Katibu Tawala Mkoa wa Singida Liana Hassan.
Katibu Mahsusi Mwanahamisi Binde akiandaa keki kwa ajili ya wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida.
Afisa utumishi Fransisca Mmari akisherehesha shughuli ya kumpongeza Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw Liana Hassan kwa kutimiza umri wa miaka 59.


No comments:

Post a Comment