Mkuu wa mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego amezungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari leo Aprili 23,2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kusogeza upatikanaji wa matibabu katika maeneo ya vijijini
Amesema kwa awamu ya kwanza huduma hiyo inatarajia kuanza kutolewa tarehe 28.04 hadi 03.2025 na kuwataka wananchi kujitokeza kwenye hospitali ziliopo katika halmashauri zao.
Pia,Amesema kutakuwa na madaktari na wauguzi bingwa 49 wa magonjwa ya watoto, magonjwa ya uzazi na wanawake, upasuaji wa jumla, huduma ya usingizi na ganzi, Magonjwa ya pua koo na masikio,huduma za kinywa na meno na huduma za uuguzi na kinga.
Dendego Amefafanua kuwa katika awamu ya pili kutakuwa na huduma itakayoanza tarehe 05 hadi 09,2025 ambapo madaktari 55 watatoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Singida.
Hatua hiyo ikilenga kuwatibu wagonjwa waliopewa rufaa katika awamu ya kwanza katika halmashauri mbalimbali mkoani Singida.
“Kutakuwa na madaktari bingwa na bobezi 55 katika fani 16 zinazogusa magonjwa ya ndani, wanawake na uzazi,watoto, upasuaji, upasuaji wa mifupa,njia ya mkojo,macho, masikio pua na koo,urekebishaji wa kinywa na meno, radiologia, usingizi na ganzi,urekebishaji wa kinywa na meno,utengemeo na viungo, mishipa ya fahamu na ubongo,ubingwa na ngozi, afya ya akili,na urekebishaji wa viungo;”alisema Dendego.
Aidha amewataka wananchi wenye magonjwa yaliyotajwa wajitokeze katika hosptali iliyopo kwenye Halmashauri zao ili kukutana na madaktari kwa kusikilizwa na kupatiwa tiba.
“Niseme wananchi wote mhakikishe mnafika mapema mtakuta timu hizo zimejipanga ili ziweze kuwashugulikia ,” Amesema Mhe.Dendego
Pia Amesema mkoa wa Singida unaendelea kumshukuru Rais Dr Samia Suluhu Hasan kwa kusogeza huduma karibu na kuwaepushia wagonjwa kwenda mbali kutafuta matibabu
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa,Dkt.Victorina Ludovick amesema kwenye Hospitali ya rufaa ya Mkoa wanatarajia kuwafikia watu takribani elfu tatu na huku kila Halmashauri wakitarajia kufikia zaidi ya watu elfu nne.
VIDEO:
No comments:
Post a Comment