Tuesday, January 23, 2024

RC SERUKAMBA AZITAKA HALMASHAURI MKOANI SINGIDA KUKIPA KIPAUMBELE KILIMO...


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, ametoa wito huo leo tarehe 23 January, 2024 wakati wa kikao kazi cha kuhimiza ugawaji wa mbegu, mbolea na uandikishaji wa wanafunzi mkoani humo.

Serukamba amesema ili Halmashauri ipate mapato lazima iwe na vyanzo ambapo ameeleza moja ya chanzo ni mazao yanayotozwa kupitia kwenye mageti ya tozo hivyo ni vyema maafisa kilimo kuhakikisha wakulima wanapatiwa mbegu bora na mbolea kwa wakati ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kilihusisha Wakuu wa Wilaya, Kaima Katibu Tawala Mkoa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, Afisa Elimu Mkoa, Katibu Tawala wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi pamoja na Maafisa Kilimo .

No comments:

Post a Comment