Viongozi wa Halmashauri zote za Mkoa Singida
wametakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria Wazazi wote ambao hawajawapeleka
watoto wao wenye sifa za kuanza Darasa Kwanza na wale wanaotakiwa kuripoti
kuanza Kidato cha Kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba,
alitoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Kizonzo wilayani Iramba Mkoani humo.
Serukamba alisema ni lazima kila mtoto
mwenyewe sifa za kuanza Darasa la Kwanza na wale waliofaulu kujiunga na Kidato
cha Kwanza wanaanza shule mara moja.
Alisema endapo mzazi au mlezi ataonekana kuwa
kikwazo cha mtoto kuanza shule ni lazima achukuliwe hatua kali za kisheria
ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani.
Aidha alisema kutokuwapeleka watoto shule ni
kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata Elimu, ambayo kwa sasa serikali
imeboresha miundombinu ya Elimu na kutoa elimu bila Malipo.
Hata hivyo Serukamba amewahimiza wananchi
kuendelea kuutumia msimu huu wa Kilimo kuongea juhudi zaidiqq katika shuguli
hizo za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa Mazao mbalimbali.
Alisema ili kuongeza uzalishaji wa Mazao, ni
muhimu kwa wakulima kutumia Mbegu Bora na kuongeza matumizi ya Mbolea.
Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kizonzo
walisema kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa
huduma ya maji safi na Salama, hali inayowalazimu akina Mama kutembea umbali
mrefu kufuata Maji kwa kutumia muda mrefu.
Kutokana na changamoto hiyo wananchi hao wameiomba serikali
kuwapatia huduma ya maji kwa kusambaza maji katika vitongoji vyote vya kijiji
cha Kizonzo.
Wananchi hao pia wameongeza kuwa kijiji hicho
hakina Zahanati na kusababisha akina Mama na watoto kupata changamoto ya
kufuata huduma za Afya umbali mrefu.
Walisema kukosekana kwa Zahanati kijijini
hapo, imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa akina Mama wajawazito, hali
inayosababisha baadhi ya akina Mama kujifungulia Njiani wakifuata Zahanati
vijiji vya jirani.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo
ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kukagua ujenzi wa
Zahanati kijiji cha Mukulu, kukagua ujenzi wa darasa moja shule ya msingi
Mgongo, ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Sherui, Zahanati kijiji cha Mseko,
amekagua ujenzi wa daraja la Mkima na Kituo cha Afya Mto Wilayani Iramba.
No comments:
Post a Comment