Monday, January 08, 2024

RC SERUKAMBA AJA NA MBINU MPYA KUHAKIKISHA MKULIMA WA SINGIDA ANANUFAIKA...


Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo tarehe 8 Januari, 2024 amefanya ziara katika Halmashauri ya Iramba na Mkalama ili kuhamasisha kilimo bora chenye tija kwa kuhakikisha Maafisa Kilimo wanatoa elimu ya mbinu bora za kilimo cha kisayansi ili kuongeza uzalishaji pamoja, kumuwezesha Mkulima kupata mavuno mengi ili kuongeza kipato pamoja na Halmashauri kupata mapato yatokanayo na kilimo.

Aidha, Maafisa Kilimo kuhakaikisha kila mkulima ananufaika na kilimo chake, Kupima afya ya udongo kwenye mashamba ili kuweza kumshauri mkulima zao la kulima, kila ifikapo mwisho wa mwaka kutathimini hali ya kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji, Serukamba amewataka Maafisa Kilimo kutembelea mashamba na wakulima kupatiwa elimu ya kilimo bora sambamba na matumizi ya mbegu na mbolea. Madiwa kuhamasisha wakulima na ikiwezekana kuwa mfano angalau kulima hata ekari moja yenye tija.
Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Maafisa Kilimo kukaa katika Kata wanazozisimamia ili kuwezesha upatikanaji wa ushauri wa kilimo kuwa rahisi kwa manufaa ya mkulima na halmashauri kwa kuwezesha ongezeko la uzalishaji wa mazao wenye tija.

No comments:

Post a Comment