Serukamba amesema hayo, alipokutana na Watendaji wa Kata, Vijiji na Wataalamu wa Kilimo wa Halmashauri ya itigi Wilayani Manyoni kwa lengo la kujadili msimu mpya wa Kilimo (2023/24), katika Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Itigi ili kuongeza uzalishaji wa mazao na maeneo mapya ya kilimo.
Aidha Serukamba, alitumia fursa hiyo kuwataka Maafisa Kilimo wakawahamasishe wakulima kupanda miti kwenye mipaka ya mashamba yao kama njia mojawapo ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwenye maeneo yanayowazunguka.
“Suala hili la mazingira naomba sana kila mmoja wetu atekeleze…ni muhimu pia kwa Taasisi za Serikali zikiwemo Shule, Zahanati na Vituo vya Afya kupanda miti pembezoni mwa jengo…” RC Serukamba
Serukamba amewataka Maafisa Kilimo kutoka maofisini kwenda vijijini kuelimisha wakulima umuhimu wa matumizi ya mbolea na mbegu bora ambapo amesisitiza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameleta mbolea yenye ruzuku hivyo wakulima isipowafikia ni kosa ambalo hatoweza kulivumilia kwa atakaye sababisha.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya
ya Manyoni alimshukuru Serukamba na kumhakikishia maeneo yaliyoainishwa kwenye
kikao hicho idadi ya ekari kisichopungua 4,000, zote zitalimwa na atahakikisha anasimamia
wakulima kutumia mbegu bora na mbolea, ili kuongeza uzalishaji mazao shambani.
No comments:
Post a Comment