MKOA wa Singida umedhamiria kuongeza uzalishaji wa mavuno ya zao la alizeti, kwa kuwapatia wakulima mbegu bora, kwa bei ya ruzuku, ili kuipunguzia serikali gharama kubwa kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Akifungua kikao kazi cha wadau wa zao hilo Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa huo Peter Serukamba, amewaeleza wadau wa alizeti kuwa, msimu wa kilimo wa 2022/2023, Mkoa wa Singida ulichangia asilimia 50 ya mafuta ya kula hapa nchini, hivyo msimu ujao iwapo wakulima watapatiwa mbegu bora, watachangia kwa asilimia 100.
Kikao hicho kilikuwa maalumu kwa washiriki kutoa mapendekezo ya mfumo wa soko "Stakabadhi gharani" utakaotumia kwa mazao ya alizeti na mikunde, kuanzia.mwaka 2024, na korosho kuanzia mwaka 2023.
"Ninachokata sasa wakulima wapeleke mazao yao ghalani mnunuzi akija muuzaji ataitwa ili kufanya biashara kwakufanya hivyo mkulima atanufaika kupitia kilimo, tutakaa tuweke miongozo tukisharidhika tupeleke kila Halmashauri, tukifanikiwa kwa alizeti tutaenda kwa zao lingine na watu wengi watalima". Serukamba
Aisha amesema mfumo huo utawezesha wakulima kupata kipato na Serikali kupata kodi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza na Wadau wa Kilimo mkoani Singida ili kuongeza tija katika zao la alizeti pamoja na kumuongezea kipato mkulima.
No comments:
Post a Comment