RAS amesema hayo leo (Juni 23, 2023) alipokutana na wadau wa
elimu katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambao umelenga
kuweka mkakati wa Mkoa wa kuwalinda watoto wa shule dhidi ya vitendo vya ukatili.
Amesema kamera zikiwepo katika korido ya vyoo vya shule,
madarasani na kwenye magari ya kusafirishia watoto zitasaidia kuwatia hofu
wenye nia ovu dhidi ya watoto na zitasaidia kupata ushahidi pindi watoto
wanapofanyiwa ukatili.
Pamoja na hayo Katibu Tawala ameagiza maafisa elimu
kuhakikisha vipindi vya dini shuleni vinatekelezwa kwa ufasa na watoto
kuhudhuria kikamifu na usiwe kwamba ni kwa mwanafunzi anayetaka, huku akiwataka
viongozi wa dini kuhakikisha kwamba wanakemea vitendo hivyo vya ukatili dhidi
ya watoto.
Aidha RAS amebainisha kwamba utafiti ulifanyika mwaka
2015/16 ( Tanzania Demographic and health Survey) zinaonesha kwamba 40% ya
wanawake katika umri wa miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa vitendo vya ukatili, na
10% ya wanawake wenye umri huo wamefanyiwa ukeketaji.
Hata hivyo ameeleza kwamba
utafiti mwingine uliofanyika mwaka 2009 (The Survey on violence against children) unaonesha kwamba asilimia
28 ya wasichana na asilimia 13 ya wavulana wamefanyiwa ukatili wa kingono
ambayo yametokewa maeneo ya nyumbani.
RAS Mganga ameendelea kueleza kwamba asilimia 73 ya
wasichana na 72 ya wavulana wamefanyiwa ukatili wa kimwili kati yao asilimia 60
hufanyiwa na ndugu zao.
Akimalizia hotuba yake amewaagiza maafisa elimu wote
kuhakikisha shule zote zinakuwa na madawati ya ulinzi na usalama shuleni ili
watoto waweze kujadili masuala ya ukatili.
Awali akifungua kikao kazi hicho Mganga Mkuu wa Mkoa Victorina Ludovick, alisema kikao kina lenga kuwajengea uwezo washiriki na wadau wote kutumia mbinu rafiki ya uelimishaji ili waweze kupaza sauti zao kuzuia ukatili dhidi yao.
No comments:
Post a Comment