Vijana wenye ujuzi mbalimbali Mkoani Singida wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa miradi ya Serikali ya ujenzi wa vyumba 102 vya madarasa na matundu 116 ya vyoo maeneo mbalimbali mkoani hapo kama fursa ya kujipatia ajira.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Afisa vijana wa Mkoa
huo Fredrick Ndahani alipokutana na makundi ya vijana hao katika ukumbi wa
mikutano wa Kanisa Katoliki ulioko mjini Singida.
Afisa Vijana huyo amesema Serikali imetoa jumla ya Tsh.
Bilioni 9.024 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa matundu ya vyoo,
nyumba vya walimu na ukarabati wa shule hivyo vijana watumie miradi hiyo
kuonesha uwezo wao.
Ndahani akiwa katika semina hiyo amesema vijana wasisubiri fursa
ziwafuate bali wazitafute zilipo kwa kuwa hawezi kujulikana mtu bila ya
kujitangaza huku akiwasisitiza kutumia fursa zinazotolewa na Serikali.
Aidha Ndahani amewaeleza vijana kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu
imeendelea kutoa mikopo kwa vijana yenye masharti nafuu na ambapo mpaka jumla
ya Shilingi Milioni 100.2 zimetolewa kwa vikundi vya vijana katika Mkoa wa Singida.
Saimon Mandela ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutenga muda
wa kuongea na vijana kwani vijana wengi hawajui fursa zinazotolewa na Serikali
pamoja na Miradi inayoletwa ndani ya Mkoa ambayo vijana wanaweza kuomba na
kupatiwa ajira.
Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa mwezi wa pili Katibu Mkuu CCM
Daniel Chongolo alipofanya ziara Mkoani Singida alitoa maagizo kwa vijana
kutumia vyuo vya VETA kupata ujuzi na wenye ujuzi watumike kutekeleza miradi ya Serikali badala
ya kuagiza watu kutoka nje ya maeneo husika.
No comments:
Post a Comment