Wasimamizi wa miradi ya maendeleo mkoani Singida wametakiwa kujiwekea mpango kazi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali mkoani hapo ambao utawasaidia kuandaa taarifa za utekelezaji na kuikamilisha kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga alipokutana na Wakurugenzi wa Halmashauri na wajumbe Menejimenti ya Mkoa huo ambapo amewafunda namna ya utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi.
Aidha amesema kushindwa kuwa na mpango kazi wa mradi kunasababisha taarifa kutokamilika au kukosa vigezo wakati wa kuripoti jambo ambalo linasababisha taarifa kutoeleweka kwa urahisi.
Hata hivyo amekemea utendaji wa kazi kwa mazoea jambo ambalo ameeleza kwamba halileti mafanikio na kuwashauri kuwa na ubunifu wa kila siku ili kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Mkoa huo.
"Usikubali kufanya kazi zinazofanana kila siku, jaribu kuwa mbunifu kila siku ndipo utakapoweza kutekeleza majukumu yao ki ufasaha" Dkt. Mganga.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Makatibu Tawala wasaidizi, Wakuu wa vitengo na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) pamoja na Katibu Tawala Mkoa huo Dkt. Fatma Mganga.
Baadhi ya Makatibu Tawala wasaidizi mkoa wa Singida wakiwa katika kikao.
Sehemu ya Wakuu wa vitengo na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment