Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri zote Mkoani hapo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya Lishe bila kujali kiasi cha bajeti zilizopo.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu tarehe 26.09.2022 katika Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo ambapo ilioneka baadhi ya Halmashauri zilikuwa hazijatekeleza kiashiria cha kutenga fedha kwa ajili ya Lishe.
Serukamba amesema kama Halmashauri hazitaweza kutenga fedha hizo itasababisha kuongezeka kwa changamoto zinazosabisha lishe duni ikiwemo udumavu wa akili.
" Sipo tayari kuona watoto wanapata udumavu kwa kutopata Lishe Bora wakati wanachakula cha kutosha, kama Sheria imeweka utaratibu wa kutenga kiasi cha TSH.1000 kwa kila mtoto inakuaje Halmashauri isitekeleze agizo hilo? hii haikubaliki" Alisema
Aidha amewataka wataalamu wa Lishe kuaandaa vipeperushi na viwekwe katika Hospitali na Zahanati na vigawanywe kwa mama wajawazito na mama wanyonyeshaji vitakavyoonesha namna ya kuandaa vyakula vya watoto na wajawazito ili kuondoa tatizo la utapia mlo.
Hata hivyo Serukamba akabainisha kwamba Vikao vya kimkoa na vya Wilaya lazima vikae na kujadili mambo muhimu ya kijamii ikiwemo na la Lishe, na taarifa ipelekwe ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili tuweze kuona na kuimarisha Afya za watoto.
Aidha amewataka waganga wakuu wa Wilaya kuwatumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii katika kuwabaini watoto wenye changamoto ya utapia mlo na kuwahudumia.
No comments:
Post a Comment