Friday, July 15, 2022

Pimeni viwanja muwauzie wananchi kwa Bei ndogo- Waziri Mkuu

Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Mkoani Singida  imeagizwa kupima viwanja vya gharama nafuu katika maeneo yanayozunguka eneo la shule mpya ya wasichana ya Soliya iliyopo Wilayani hapo ili kuongeza kasi ya maendeleo katika mji huo.

Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Manyoni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika shule hiyo ambapo aliiagiza Halmashauri hiyo kupima viwanja maeneo hayo na kuviuza kwa bei ndogo kama gharama ya upimaji.

Amesema eneo hilo linahitaji kuendelezwa kwa kuhakikisha miundombinu ya maji Umeme Barabara za mitaa vinakuwepo ili kuendeleza eneo hilo.

Awali Waziri Mkuu aliagiza Ujenzi huo uliogharimu Tsh. Bilioni  tatu kukamilika kwa wakati na kwa ubora uliotarajiwa ili waweze kuchukua wanafunzi wapatao 600.

Ziara hiyo ya waziri mkuu imeanza Leo 15/7/2022 na itaendelea mpaka tarehe 19/7/2022

Matukio katika picha katika shule ya Sekondari ya Wasichana Solya.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akishiriki uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya Sekondari Solya wilayani Manyoni.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa kukagua ujenzi wa Shule.



Ziara ikiendelea

Moja ya jengo la shule ya Sekondari ya Wasichana Solya ambako ujenzi unaendelea

No comments:

Post a Comment