Wakulima wa alizeti Mkoani Singida wapo mbioni kunufaika na mfumo wa M-Mkulima ambao umelenga kutoa taarifa sahihi zinazohusiana na kilimo ikiwemo hali ya hewa Bima ya mazao mikopo na ushauri.
Akiongea wakati wa Mafunzo kwa Maafisa ugani wa Wilaya ya Ikungi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, Meneja wa mifumo ya kidijitali na Intanent ya vitu kutoka Kampuni yaVodacom Mike Kasungu amesema mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa ambazo zitasaidia wakulima kukopesheka benki na kuongeza tija ya Kilimo chao.
Wakulima wengi walikuwa hawakopesheki kwa sababu mabenki walikuwa hawana taarifa sahihi za mkulima lakini kupitia mfumo wa M-Mkulima utakuwa na taarifa za mkulima kuhusu aina ya mazao anayolima, ukubwa wa shamba na masoko yaliopo. Alisema Mike Kasungu.
Make amesema mfumo ulianzia Kanda ya ziwa kwa wakulima wa pamba ambapo mafanikio yalikuwa makubwa na bado wakulima wengi wamekuwa wakijiunga kupitia Maafisa ugani wao.
Amesema kwa sasa Kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo wanatoa elimu kwa Maafisa ugani katika Kanda ya Kati hasa Mkoa wa Singida kuhusiana na namna ya kuwasajili wakulima wa alizeti katika mfumo Mkoani hapo ili waweze kupata taarifa kuhusu mbinu Bora za kilimo, Bima za mazao, masoko na mikopo kwa ajili ya shughuli zao za kilimo.
Baadhi ya Maafisa Ugani wa Wilaya ya Ikungi wakiwa katika mafunzo hayo
Hivi karibuni Waziri wa kilimo Husein Bashe akiwa Bungeni alibainisha kwamba Serikali imedhamiria kubadilisha kilimo kuwa cha ki biashara ili kiweze kuwa na tija kwa wakulima.
Bashe alieleza kwamba moja ya changamoto ya wakulima ni kukosa taarifa muhimu za kilimo kama hali ya hewa upatikanaji wa pembejeo za kilimo na taarifa za soko jambo ambalo Wizara hiyo inalishughulikia kupitia njia mbalimbali za Kiserikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
Alisema kwamba mikakati mbalimbali inafanyika ili mkulima aweze kutambulika na kukopesheka kupitia mabenki jambo ambalo ndilo Kampuni ya Vodacom inalolifanya kupitia mfumo wa M-Mkulima alieleza Waziri wa Kilimo.
No comments:
Post a Comment