Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge leo ametembelea
masoko ya Kilambida, Mitunduruni na Mahembe yaliyopo katika Manispaa hiyo lengo likiwa ni kukagua mazingira ya
usafi pamoja na maeneo waliyokwisha pangiwa kufanyia biashara ya mazao ya
chakula.
Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa huyo akamuagiza
Mkurungezi wa Manispaa ya Singida kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa wamiliki wa makaburi yaliyopo soko la mahembe ili
kupisha wafanyabiashara pamoja na
kufanya marekebisho ya miundombinu
katika baadhi ya maeneo hayo.
Aidha Dk. Mahenge kasisitiza ujenzi wa maegesho ya magari na sehemu za kushushia mizigo pamoja na kulifanya soko la Mahembe kama sehemu ya kushushia ndizi na viazi kutokana na maeneo mengine kuwa yameshajaa.
Dk. Mahenge akaendelea kuitaka Manispaa kuhakikisha wananchi
wanapata taarifa ya kila kinachoendelea
kuhusu fidia za makaburi na baadhi ya wamiliki wa nyumba ambazo
zinatakiwa kupisha eneo la soko na kuwataka kuweka utaratibu ambao hautachelewesha
utekelezaji wa shughuli hizo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili
akawataka wafanyabiashara hao kuhakikisha kwamba wanabaki katika maeneo yao
waliyopangiwa wakati serikali ikiendelea kupambana na changamoto
zinazojitokeza.
Aidha DC Muragili akawataka viongozi wa masoko kuelimishana
ili kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya masoko
ikiwa ni pamoja na kukubali kufanya maendeleo wakati taratibu za malipo ya
fidia yakiendelea.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Dk.
Adrianus Kalekizi amemueleza Mkuu wa Mkoa kwamba Manispaa imejipanga
kuhakikisha zoezi litakamilika ifikapo
mwezi Mei 2022 ambapo kwa sasa tayari
bajeti yake imeshapangwa.
Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa iliwahusisha Viongozi wote wa
Manispaa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wataalamu mbalimbali wa
mazingira.
No comments:
Post a Comment