Mkoa wa Singida umejipanga kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kuondoa daraja la mwisho (sifuri) katika shule za sekondari kwa kuanzisha mfumo wa kufundishia masomo ya sayansi kwa shule ambazo zina uhaba wa walimu wa masomo hayo.
Akizungumza wakati wa majaribio ya kufundisha kwa kutumia
mfumo huo wa kijiditali yaliyofanyika hivi karibuni katika Shule ya Sekondari
Mitunduruni iliyopo Manispaa ya Singida, Katibu Tawala Mkoa huo Bi Dorothy
Mwaluko amesema Mkoa umepanga kuongeza uelewa na ufaulu kwa wanafunzi wa
Sekondari kwa kutumia video zilizohifadhiwa kwenye vifaa mbalimbali kama flash
ili kufundishia mashule ambayo hayana walimu wa masomo hayo.
Katibu Tawala huyo amesema kufundisha kwa njia ya video
kunamfanya mwanafunzi kuelewa kwa haraka kupitia njia tatu za ufahamu ambazo ni
macho kuona, masikio kusikia na kuhisi kwa kugusa au kuandika na kuwataka
walimu wa masomo hayo kujiandaa kutumia mfumo huo wakati marekebisho kadhaa ya
kuuboresha yanafanyika.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza na wanafunzi
Aidha Dorothy amebainisha kwamba jumla ya shule 142 za
Serikali ndizo zitakazofaidika na mfumo huo
hasa zenye walimu wachache wa masomo ya sayansi kama hisabati phizikia
na Kemia.
“Mfumo huo unatazamiwa kutumika mara tu mapendekezo ya
maboresho ya mfumo yaliopendekezwa na walimu na wanafunzi wa shule hii na
nyengine zitakazopata bahati yakufanyiwa majaribio”. Alisistiza Mwaluko.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Mitunduruni Mwalimu Victoria
Calist akishukuru ujio wa programu na shule hiyo kuchaguliwa kuwa ya kwanza
kufanyiwa majaribio hayo, amesema mfumo utawasaidia shule ambazo hazina walimu
wa masomo husika na kukazia maarifa kwa shule ambazo tayari wanawalimu.
Amesema kwa mkoa wa Singida kuna upungufu mkubwa wa walimu wa
masomo ya Sayansi yakiwemo hisabati na phizikia jambo ambalo lilikuwa likipunguza
ufaulu wa wanafuzi hivyo uwepo wa mfumo huo utaondoa changamoto hiyo.
Aidha Mkuu wa Shule huyo akaomba wataalamu wa TEHAMA kusaidia video
kupatikana kwa njia ya flashi au DVD ili
wanafunzi waweze kujifunza wakiwa majumbani au mashuleni .
Hata hivyo Mwalimu Victoria alimshuku Afisa Tawala Mkoa
pamoja na Mkuu wa Mkoa Dk. Binilith Mahenge kwa
ubunifu huo ambao utasaidia
kuondoa changamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi mkoani Singida.
Silivanus Mputa ni mtaalamu wa TEHAMA ambaye alishirikiana na
Afisa TEHAMA wa Mkoa Bw. Baraka Mhembano katika utengenezaji wa mfumo huo hapa
anasema, utengenezaji wa mfumo huo wa kufundishia kwa kutumia video na sauti
kwa sasa wamefanikiwa kutengeza vipinda vya masomo ya Hisabati Kiswahili na
Baiolojia ambayo ndiyo yaliyotumika kufanyia majaribio.
Silivanus amefafanua kwamba vipindi hivyo vimegawanyika
katika sehemu tatu (3) ikijumuisha
vilivyotengenezwa kwa kuonesha picha na sauti (real class) ambapo
Mwalimu anafundisha kwa kuonekana, njia ya pili ni vilivyotengenezwa kwa njia
ya wasilisho ambavyo vinakuwa na maandishi picha za mnato na sauti.
Njia nyingene ni video amabazo zimetengenezwa kwa njia ya
uhuishaji (animation) ambazo zote zimetengenezwa na program mbalimbali ikiwemo
adobe Premiere na Adobe photoshop. Alifafanua Silivanus.
Katika zoezi la kutumia mfumo wa kufundishia wanafunzi wa
sekondari umehusisha wanafunzi wa shule
ya Mitunduruni iliyopo Manisiapaa ya Singida ambapo Aisha Haji Abdalah
mwanafunzi wa kidato cha nne A akaishukuru Serikali ya mkoa ambayo imepanga
kuboresha elimu.
Aisha ameeleza kwamba matumizi ya mfumo wa kufundishia masomo ya sayansi kwa shule za sekondari umeonesha wazi kwamba nchi ipo katika uchumi wa kati ambao unahitaji matumizi ya teknolojia katika kusambaza na kukuza maarifa kutoka mtu moja hadi mwingine.
No comments:
Post a Comment