Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida leo wamejengewa uwezo wa uwekaji wa akiba fedha zao kupitia kampuni ya UTT AMIS inayohudumia mifuko mbalimbali ikiwemo mfuko wa umoja, wekeza maisha, mfuko wa watoto na mfuko wa kujikimu.
Akieleza umuhimu wa kuwekeza katika mifuko iliyoanzishwa na
ATT AMIS muendesha mada Bi Grace Ngairo kutoka Taasisi ya UTT AMIS iliyo chini
ya Wizara ya fedha amewahamasisha watumishi kujiunga na mifuko hiyo kwa kuwa
kampuni hiyo inaendeshwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya uwekezaji.
Aidha Grace amesema mifuko hiyo ni rahisi kufuatitia mienendo
ya masoko kwa mteja na wawekezaji wanafaidika pamoja na unafauu wa gharama za
uwekezaji.
Akiendelea na wasilisho lake kwa watumishi hao Grace
akabainisha kwamba kupitia mfuko wa taasisi hiyo mwekezaji anapunguza hatari za
uwekezaji kwa kuwekeza katika uwekezaji anuai ambapo alibainisha kwamba mfumo
huo ni rahisi kujiunga.
Aidha amewashauri watumishi hao kupunguza matumizi yasiyokuwa
ya lazima huku akiwafundisha kutenga asilimia 10 hadi 20% kwa fedha yeyote
wanayoipata ili kuongeza uwekezaji kwa maisha ya baadae.
Naye Kaimu Afisa Tawala wa Mkoa huo Bwana Justo Hermani
akitoa shukrani kwa watoa mada hao amewataka watumishi kujitafakari kwa mafunzo
waliyoyapata na kuaanza kuwekeza kwa ajili ya maisha yao ya baadae na watoto
wao.
Bwana Justo akabainisha kwamba uwekezaji huo utawasaidia
watumishi ambao wengi wao wamewekeza kwenye ujenzi wa majumba na ununuzi wa
magari ambao amesema mali hizo huchukua muda mrefu kuuzika pindi mtumishi anapopata
dharura kuliko fedha uliyowekeza.
Kwa upande wake Bwana Peter Kashindye moja ya watumishi waliohudhuria mafunzo hayo ameshukuru ujio wa wataalamu hao ambao ameeleza kwamba uwekezaji uliofundisha utasaidia katika kujipanga kusomesha watoto kwa urahisi na kujiandalia maisha ya baadae.
No comments:
Post a Comment