Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge hivi karibuni
amekutana na Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia maandalizi ya Ujenzi wa Chuo cha
Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) ambacho ni
Kampasi ya Singida.
Wakiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Naibu waziri huyo amasema lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli za
Ujenzi wa chuo hicho na kutembelea shughuli za TASAF zinazoendelea Wilayani
Manyoni.
Amesema Chuo hicho kitakuwa ni msaada mkubwa kwa watu wa
Singida na maeneo mengine huku alibainisha kwamba uchumi utapanuka na ajira
zitaongezeka.
Kwa upande wake RC. Mahenge ameshukuru Ujenzi wa chuo hicho na kusema ni hatua kubwa
ya maendeleo kwa Mkoa huo.
Aidha amemuomba Naibu waziri huyo kushughulikia changamoto ya
watumishi wa Mkoa huo ambao wamekuwa wakikaimu kwa muda mrefu pasipo kuthibitishwa.
Hata hivyo RC akamueleza Naibu Waziri huyo changamoto ya
uhaba wa walimu na madaktari Katika Mkoa huo huku akibainisha kwamba ongezeko
la madarasa na vituo vya Afya vilivyomalizika hivi karibuni kumeleta uhitaji
mkubwa wa walimu na manesi.
No comments:
Post a Comment