Monday, November 15, 2021

TUTAIFANYA SINGIDA MJI WA KUPUMZIKIA - DKT MAHENGE

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ametoa maagizo kwa Wakuu wa Taasisi za TANESCO, wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA), wakala wa barabara (TANROAD) na Manispaa  ya mji wa Singida kupanda miti katika maeneo yote muhimu  na kutengeneza maeneo ya kupumzikia kwa lengo la kubadilisha mandhari ya mji wa huo.

Akiongea wakati wa kikao hicho kilichofanyika 15/11/2021 ofisini kwake Dkt. Mahenge amesema umefika wakati wa kuubadilisha mji wa Singida kwa kuwa umekuwa ni makutano ya kibiashara kutoka pande zote za nchi hivyo kufanya kuwa eneo la kupumzikia.

Aidha RC Mahenge ameagiza ujenzi wa vimbweta katika fukwe za maziwa ya Kindai na Singidani, katikati ya mji na pembezoni  pamoja na upandaji wa miti kuzunguka maeneo hayo jambo ambalo litasidia kuboresha mazingira na kuleta hewa safi pamoja na vivuli .

Kikao kazi hicho kilipanga kuwakutanisha  Mkurungezi wa Manispaa, TARURA, TANESCO, TANROAD, Wakala wa Bonde, VETA na Magereza ambapo Mkuu wa Mkoa amebainisha kwamba huko ndipo penye rasilimali za kufanikisha kazi hizo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wawakilishi wa Taasisi hizo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa jitihada zake za kuubadilisha mkoa wa Singida  na kuahidi kwamba watakutana na kufanya kikao kidogo cha kukubaliana namna ya utekelezaji wa maagizo hayo na kuanza kazi mara moja

Hata hivyo wamebainisha kwamba uboreshwaji wa mazingira hayo kutasaidia utunzaji wa mazingira na kuvutia wawekezaji ambapo biashara za ndani na nje ya mkoa zitakuwa endelevu.



No comments:

Post a Comment