WAKUU wa Idara mbalimbali mkoani Singida wametakiwa kuongeza ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha kazi wanazofanya zinawafikia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko katika kikao chake na Watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida.
Katika kikao kazi hicho kilichowahusisha Watumishi wote kilikuwa cha kukumbushana majukumu ya kila mmoja na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake watumie utaalamu kukamilisha majuku yao.
Aidha Mwl. Dorothy amesema mkoa una fursa nyingi ambazo hazijafahamika vizuri kwa Watanzania walio wengi na kuwataka wakuu wa Idara kushirikiana na vyombo vya habari ili kujitangaza zaidi
Aidha, Katibu Tawala Mkoa amewapongeza wakuu hawa wa Idara na Watumishi kwa ujumla kwa namna wanavyofanya kazi na kuwataka kuongeza juhudi kwakuwa wana uwezo wa kufanya kazi nzuri zaidi ya hiyo.
Pamoja na mambo mengine Katibu Tawala Mkoa huyo amewataka watumishi wote kuhakikisha wanatunza mali za umma ili ziweze kufanya kazi zilizotegemewa na kuwaletea wananchi manufaa.
mwisho
No comments:
Post a Comment