Mkuu wa
mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, amezindua mashindano ya Umoja wa Michezo
kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha
wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Akizindua
mashindano hayo, Mkuu wa mkoa wa SINGIDA Dkt. REHEMA NCHIMBI amehimiza suala la
nidhamu kwa wachezaji na kusisitiza kuwa
anaimani kuwa wachezaji watakaochaguliwa kwenda kuuwakilisha mkoa kwenye
mashindano ya taifa yatakayofanyika mkoani Mtwara watafanya vizuri ili kuibuka
na medali nyingi na kuuletea heshima mkoa wa SINGIDA.
Dkt.
Nchimbi amesema, Michuano hii ndio itakuwa chemichemi ya kuchagua wachezaji ambao wataenda kuuwakilisha mkoa wa
SINGIDA katika michuano ya Umisseta ngazi ya Taifa huko mkoani MTWARA na
Viongozi wa mkoa wa SINGIDA wamesema wanaimani kubwa kuwa timu ambayo
itachaguliwa itakuwa bora na itafanya vyema kwenye michuano hiyo.
"Hatuna timu nyingine, timu
ni hii hapa, ninyi ndio timu yetu ya mkoa wa Singida. mimi sina timu nyingine,
na sio timu ya mzaha ni timu ya ushindi"
"Mnauwezo, na lazima mkafanye
vizuri, mtakapo kuwepo na sisi tupo. tunachotaka ni kimoja tuu... ushindi.
" Amesema Dkt. Nchimbi
Kwa upande
wake Katibu Tawala wa mkoa wa Singida Dkt.
ANGELINA LUTAMBI akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema, mwaka huu
mkoa wa Singida umejipanga vizuri katika michuano hiyo ya UMISSETA na kuwataka
wachezaji wote walioingia kambini hapo kucheza kwa bidii na nidhamu ya hali ya
juu katika michuano hiyo ili kujitangaza na kuuletea sifa mkoa wa Singida
katika sekta ya michezo nchini.
"Tunaamini vijana wetu
watakapo kamilisha makambi yao hapa na kwenda
kule Mtwara, mwaka huu tutafanya vizuri sana. Ninaamini kwamba
tutakapofanya vizuri katika mashindano haya, ndio itakuwa tiketi yetu yakuonekana
zaidi kitaifa". Amesema Dkt. Lutambi
Naye, Afisa
Michezo na Utamaduni wa mkoa wa Singida Bw. HENRY KAPERA amefafanua jinsi
michauno hii ilivyoibua vipaji vya wachezaji wengi ambao wengine wanasakata
kabubu kwenye timu kubwa hapa nchini.
"Kuna
wachezaji wetu walishacheza michezo ya umiseta miaka MINNE iliyopita, siku hizi
wanacheza katika vilabu vikubwa nchini akiwepo Raphael Loti aliyekuwa mchezaji
kutoka Halmashauri ya Wilaya Itigi mkoani Singida ambaye kwa sasa anayechezea
timu ya Yanga" Amesema Kapera
Pia
amemtaja Jeremia Juma anayechezea Tanzania Prisonal ambaye naye alipitia katika
michuano hiyo ya Umiseta kutoka mkoani Singida na kuwahimiza wanamichezo hao
kujituma wakati wote ili vipaji vyao vipate kuonekana na hatimaye kuwa sehemu
ya ajira.
Katika
kuhakikisha michuano hii inafanyika kwa utulivu wa hali ya juu Mkuu wa mkoa wa
SINGIDA Dkt. REHEMA NCHIMBI amechangia shilingi laki TANO kama hatua ya kuwapa
hamasa wachezaji kujiandaa vyema na michuano ya mkoa na ya kitaifa.
MATUKIO KATIKA PICHA
Wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Burudani zikiendelea wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Afisa Elimu mkoa wa Singida Mwalimu Nelas Mulungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Afisa Michezo mkoa wa Singida Bw. Henry Kapella akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari UMISSETA ngazi ya mkoa, mkoani Singida kwa kujumuisha wachezaji 700 kutoka halmashauri SABA za mkoa wa SINGIDA.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA.
No comments:
Post a Comment