Wednesday, October 03, 2018

MAAFISA TEHAMA WA HALMASHAURI ZA MKOA WA SINGIDA WAJENGEWA UWEZO KATIKA KUSIMAMIA MIFUMO NA MIUNDOMBINU YA TEHAMA KATIKA HALMASHAURI ZAO

Katika kuhakikisha Mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayotumika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inatumika ipasavyo na kuendelea kuleta matokeo chanja na kuendelea kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi kwa kutumia TEHAMA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida imeamua kufanya mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Singida katika  kusimamia Mifumo na Miundombinu ya TEHAMA katika Halmashauri zao.

Katika Mafunzo haya, Maafisa TEHAMA wa Mamlaka za Serikali za Mitaa  wanajengewa uwezo katika kusimamia mifumo yote inayotumika katika Mamlaka zao pamoja na Miundombinu ya TEHAMA.

Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wakiwa katika nyuso zenye furaha kwa kufurahia jambo wakati wakifuatilia  mada iliyokuwa ikitolewa na mwezeshaji ambaye ni Afisa TEHAMA - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Bw. Baraka Mhembano.

Washiriki wakifuatilia Mafunzo kwa makini.


 Mafunzo yakiendelea.

 Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wakiwa katika nyuso zenye tabasamu kwa kufurahia jambo wakati wakifuatilia  mada.


 Mafunzo yakiendela.

 Afisa TEHAMA , Ofisi ya Mkuu wa mkoa Singida Bw. Baraka Mhembano, akiwa anawajengea uwezo washiriki katika usimamizi wa mfumo wa kielektroniki wa uendeshaji wa Hospital (GoT-HOMIS). Sehemu ya washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za mkoa wa Singida.


 Afisa TEHAMA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Athuman Simba akizungumza wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Singida.

 Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa halmashauri za mkoa wa Singida, Bw. Salum Omary - Afisa TEHAMA Halmashauri ya Iramba  akizungumza jambo katika Mafunzo hayo.

Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Singida Bi. Eva Myula ambaye ni Afisa TEHAMA Halmashauri ya Ikungi akifuatilia mafunzo kwa Vitendo.

Mwezeshaji wa Mafunzo, Afisa TEHAMA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Singida Bw. Baraka Mhembano, akitoka katika ukumbi wa mikutano yanapofanyika mafunzo.


Afisa TEHAMA, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Bw. Baraka Mhembano (kulia) akiwa na Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Bw. Abas Said wakizungumza jambo baada ya kutoka kwenye mafunzo. Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja.

Aidha, Washiriki wameipongeza na kuishukuru Serikali ya Mkoa wa Singida kwa kuwezesha Mafunzo haya muhimu sana kwa Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kwakuwa yanawawezesha kuwa na uelewa mkubwa wa Mifumo na Miundombinu ya TEHAMA na hivyo kuisimamia vyema.IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA
SINGIDA

No comments:

Post a Comment