Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyesimama) akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku tano yanayohusu fidia kwa Watumishi ambayo yamehudhuriwa na madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya kutoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida. Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na shirika la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F.) katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Uhasibu mkoania Singida.
MKUU wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, amewataka waajiri wahakikishe wakati wote panakuwepo na mazingira rafiki mahala pa kazi kwa waajiriwa, ili kuondoa uwezekano kwa wao kuumia na kupata ulemavu au kuugua.
Dkt. Nchimbi, ametoa wito huo mwanzoni mwa wiki hii wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayohusu fidia kwa watumishi ambayo yamehudhuriwa na madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya. Walengwa hao wanatoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida. Mafunzo hayo yanaendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha uhasibu mjini hapa na yameandaliwa na kufadhiliwa na shirika la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F.).
Akifafanua, alisema mazingira mazuri ya kazi yakiwa hayana viashiria vya hatari yoyote kwa afya ya mtumishi ikiwemo kupata ulemavu au kuugua, mazingira hayo ni fidia tosha haiwezi kulinganishwa na fidia zingine zozote.
“Ni jambo jema mfanyakazi afanye kazi kipindi chote cha kuajiriwa bila kupata ulemavu wa aina yoyote au maradhi. Hili linawezekana tu endapo mazingira ya kazi yatakuwa rafiki kwa mfanyakazi”, Amesema Dkt. Nchimbi
“Ninyi ambao mnahudhuria mafunzo haya,nendeni mkawe mabalozi wazuri katika kuboresha mazingira ya kazi. Maafisa mahusiano na maafisa utumishi,pia wahakikishe mazingira ya kazi yanakuwa rafiki kwa wafanyakazi”.
Dkt. Nchimbi amewahimiza madaktari hao kufanya tathimini stahiki kwa wakati kwa wafanyakazi wanaoumia au kuugua mahali pa kazi ili waweze kulipwa fidia katika muda muafaka.
“Katika hili la fidia kwa mfanyakazi anayeumia au kupata maradhi mahali pa kazi, pasiwepo na urasimu wa aina yoyote. Muathirika ahudumiwe mapema iwezekanavyo, nisingependa pawepo na njoo kesho….njoo kesho”, Amesisitiza Dkt. Nchimbi.
Akisisitiza zaidi, Dkt. Nchimbi alisema madaktari wana dhamana kubwa kwenye suala la utoaji wa fidia. Mapendekezo yao ndiyo yanatoa muongozo kwa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kuamua ni kiwango gani ambacho muathirika anapaswa kulipwa au kutokulipwa.
Awali, Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F) Masha Msomba, alisema kati ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 na 2017/2018, wametoa fidia ya zaidi ya shilingi 4.4 bilioni kwa wafanyakazi walioimia au kupata maradhi mahali pa kazi.
Madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya kutoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Uhasibu mkoania Singida.
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F) Masha Mshomba akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) kufungua mafunzo ya siku tano yanayohusu fidia kwa watumishi ambayo yamehudhuriwa na madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya kutoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida. Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na shirika la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F.).
Daktari bingwa na mbobezi wa Magonjwa ya mifupa kutoka MOI, Dkt. Robert Mhina akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (hayupo pichani) kufungua mafunzo ya siku tano yanayohusu fidia kwa watumishi ambayo yamehudhuriwa na madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya kutoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida. Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na shirika la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F.).
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja wakati wa kufungua mafunzo ya siku tano yanayohusu fidia kwa Watumishi ambayo yamehudhuriwa na madaktari na watoa huduma mbalimbali za afya kutoka mkoa wa Dodoma, Kigoma, Tabora na Singida. Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na shirika la mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (W.C.F.) katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Uhasibu mkoania Singida.
IMETOLEWA NA;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA
No comments:
Post a Comment