Mkoa wa Singida leo umezindua
Kampeni ya FURAHA YANGU inayolenga kuhamasisha upimaji Virusi vya UKIMWI mkoani
Singida.
Akizungumza leo wakati
wa uzinduzi wa Kampeni hiyo kimkoa ambayo imefanyika katika Manispaa
ya Singida, Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi amesema
Kampeni ya Furaha Yangu imejikita zaidi
katika kutoa hamasa kwa wanaume na wananchi walio katika mazingira hatarishi ya
kupata maambukizi ya VVU na kwenda kupata huduma ya ushauri na upimaji wa VVU
na kuanza dawa mapema kama atakuwa amegundulika anaishi na maamukizi ya VVU.
Dkt. Nchimbi amesema,
Kampeni hii itasaidia juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambazo ni kufikia malengo ya 90 tatu kama ilivyoelekezwa na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS.
“Hii inamaanisha
kwamba, mpaka kufikia mwaka 2020, asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi wafahamu kuwa wanaishi na VVU, asilimia 90 ya wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI watumie ARV kwa usahihi na uendelevu na asilimia 90 ya wanaotumia ARV
waweze kufubaza Virusi Vya UKIMWI” Dkt. Nchimbi.
Amesema katika
kufikia malengo haya, ni muhimu kwa Mkoa wetu wa Singida kila mtu akatimiza
wajibu wake licha ya kwamba bado hali ya maambukizi katika mkoa wetu ni
asilimia 3.4 ambayo ipo chini ya kiwango cha kitaifa (4.7%), kwa mujibu wa
utafiti wa Viashiria vya UKIMWI hapa nchini vya mwaka 2012.
Aidha, amewaagiza
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote saba za mkoa wa Singida, kuhakikisha
wanashirikiana na wadau mbalimbali kutenga maeneo ambayo wananchi watakwenda
kupata ushauri na kasha kupima, na kama watagundulika kuwa na maambukizi waanze
matibabu mapema kwa ajili ya kuwafanya wafurahie maisha.
“Naamini kwa kufanya
hivi, Kampeni hii itafanikiwa na itachangia Dira yetu ya Singida bila UKIMWI
inawezekana. FURAHA YANGU – PIMA, JITAMBUE, ISHI” Dkt. Nchimbi.
MATUKIO KATIKA PICHA
Kamishna Msaidizi idara ya Uhamiaji Mkoa wa Singida Bi. Angela Shija akizungumza akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Daktari Sisty Joseph Moshi kutoka Tanzania Health Support akizungumza kwa niaba ya wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mganga Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Victoria Ludovick akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Bw. Emmanuel Luhaula akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jackson Masaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na mwanamuziki Tunda Man aliyetumbuiza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pasacas Muragiri akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Huduma zikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kulia) akimpongeza mwanamuziki maarufu nchini Tunda Man mara baada ya kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika kufanikisha uzinduzi wa Kampeni ya FURAHA YANGU mkoani Singida.
Imetolewa na ;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA
No comments:
Post a Comment