Saturday, September 15, 2018

MKUU WA MKOA SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AKABIDHI PIKIPIKI KWA WARATIBU WA ELIMU NGAZI YA KATA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA SINGIDA LEO 15/09/2018


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwasha moja ya pikipiki ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia Waratibu Elimu ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya Singida, mkoani Singida mapema leo ili kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu mkoani Singida.




Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ugawaji wa pikipiki kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata katika halmashauri ya Wilaya ya Singida wakati wa hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya Singida, mkoani Singida leo. Kutoka kulia ni Kiongozi wa EQUIP mkoa wa Singida Mwl. Phoebe Okeyo, Afisa Elimu mkoa Singida Mwl. Nelasi Malungu, Mkuu wa wilaya Singida Bw. Pasacas Muragiri.








 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikabidhi funguo pamoja na kofia ngumu kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambao wamepatiwa pikipiki kwa ajili ya kusimamia sekta ya elimu.

 Pikipiki aina ya Honda zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya Maafisa Elimu Kata wilaya ya Singida leo mkoani Singida.







 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa nne kutoka kulia waliosimama) akiwa pamoja na mkuu wa wilaya ya Singida Bw. Pasacas Muragiri (katikati), Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Bw. Elia Digha pamoja na Afisa Elimu mkoa Mwl. Nelasi Malungu wakishuhudia zoezi la mkataba wa makabidhiano ya pikipiki aina ya Honda kati ya halmashauri ya wilaya ya Singida na Waratibu wa Elimu kata wa hamlashauri ya wilaya Singida.









  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikabidhi hati ya mkataba wa makabidhiano ya pikipiki kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambao wamepatiwa pikipiki kwa ajili ya kufuatilia na kusimamia shughuli za sekta ya elimu kata katika halmashauri ya wilaya Singida, mkoani Singida.


  Mmoja kati ya Waratibu wa Elimu Kata katika halmashauri ya wilaya Singida akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waratibu wa halmashauri kwa Mheshimiwa Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwaniaba ya Serikali ya awamu ya tano.



  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambao wamepatiwa pikipiki kwa ajili ya kufuatilia na kusimamia shughuli za sekta ya elimu kata katika halmashauri ya wilaya Singida, mkoani Singida.


  Afisa Elimu mkoa Singida Mwl. Nelasi Malungu akizungumza.

  
   Kikao kikiendelea

 Mkuu wa wilaya Singida Bw. Pasacas Muragiri akizungumza na waratibu wa elimu kata halmashauri ya wilaya ya Singida.


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Singida Bw. Rashidi Mandoa (kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya Singida Bw. Wilson Shimo wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki kwa waratibu wa elimu kata halmashauri ya wilaya Singida mkoani Singida.

    Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza.

KATIKA HATUA NYINGINE 
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya aliweza kusimamisha msafara wake kwa muda ili kusalimia na kutoa neno kwa Waratibu wa Elimu Kata halmashauri ya wilaya Singida alipokuwa katika ziara (Kongano)  leo mkoani Singida.


 

  Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akizungumza na Waratibu wa Elimu ngazi ya Kata katika halmashauri ya wilaya ya Singida wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa waratibu wa elimu kata halmashauri ya wilaya Singida leo mkoani Singida



 Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya (kulia) akiongoza zoezi la kuipongeza Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kuwajali, kuwathamini na kuwapenda Walimu nchini kwa kutoa pikipiki wa Waratibu wa Elimu nchini.
 Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya (kulia) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ili kuendelea na ziara leo mkoa Singida.

Mkoa wa Singida umesambaza jumla ya pikipiki 136 kwenye Halmashauri zake 7 ambapo Ikungi 28, Iramba 20, Itigi 13, Manyoni 19, Mkalama 17,
Singida 21 na Singida MC 18.

Imetolewa na 
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
SINGIDA

No comments:

Post a Comment