Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi mapema leo akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya
kupanga miradi ya maendelo kwa jamii yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za
mkoa wa Singida, kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi.
Naibu Mshauri Mkuu, Maendeleo ya Mfumo
wa Mafunzo wa Mpango Shirikishi Jamii kutoka shirika la JICA Naoyuki Shintani
akiwa na Mtaalam wa mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo O&OD kutoka OR-TAMISEMI
Silas Salamaluku wakijadilia jambo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa
halmashauri za Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya
Iramba Linno Mwageni na baadhi ya
watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya
kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD)
yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za
Mitaa Mwajabu Nyamkomola na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt.
Mpamila Madale wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa
ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na
ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji
wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi Rustika Turuka baadhi ya watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida
wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya
kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri
zote za mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema
Nchimbi amezitaka halmashauri za Mkoa wa Singida kuacha kulalamika kukosa mapato
bali watumie vizuri rasilimali nyingi zilizopo, ambazo zikitumika vizuri
zinaweza kuongeza mapato yao.
Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema leo
wakati akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga
miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za
mkoa wa Singida.
Amesema Mkoa una fursa nyingi katika
sekta ya kilimo, utalii, ufugaji, madini na uvuvi ambazo bado hazijatumiwa
vizuri na halmashauri katika kukuza uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya
Mkoa wa Singida.
“Singida ina zalisha Vitunguu vingi na
bora nchini, ina zalisha viazi zitani vingi na vyenye ubora, singida pia ni
mzalishaji mkubwa wa alizeti na mafuta ya alizeti huku tukiwa na viwanda zaidi
a 120 vya kusindika mafuta ya alizeti, katika sekta ya utalii tuna vivuti vngi
ikiwemo bwawa la kuongelea ‘swimming pool’ lililojengwa na mjerumani na lipo
katikati ya pori lakini vyote hivi hatujavitumia vizuri,” amesisitiza Dkt
Nchimbi.
Dkt Nchimbi ameongeza kuwa halmashauri
zinapaswa kutotumia mafunzo hayo kulalamika bali mafunzo hayo yawajengee uwezo
wa kutambua wapi kuna pengo katika maendeleo ya jamii na kisha kuanisha fursa
na mikakati ya kuzitumia fursa hizo kuziba pengo hilo.
Aidha amewataka kutumia fursa ya
malengo na mitazamo waliyonayo ambayo inaweza kuleta maendeleo pamoja na
kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kubaini na kuitumia ajenda
ya fursa na vikwazo katika maendeleo kwa ngazi zote.
Dkt Nchimbi amesema matarajio yake ni
kuona kila mshiriki wa mafunzo hayo ana mabadiliko ya tabia katika utendaji
wake ambapo mabadiliko hayo yanaweza kupimika aidha kwa macho au viashiria
vingine.
Ameongeza kuwa matarajio ya mengine ni
kuwa na Singida mpya yenye takwimu sahihi za bidhaa zote zinazozalishwa Mkoani
Singida ili kuzitumia takwimu hizo katika kupanga mikakati ya maendeleo pamoja
na kutangaza fursa zote zilizopo Mkoani hapa.
Dkt Nchimbi ameeleza kuwa mafunzo hayo
wamepatiwa ili kutatua changamoto zilizopo na endapo kutaendelea kuwepo kwa
changamoto hizo katika sekta mbalimbali ikiwemo za kilimo, afya, maji, elimu,
barabara na utawala bora basi tumi nzima ya fursa na vikwazo itakuwa imeshindwa.
No comments:
Post a Comment