Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Rehema Nchimbi akishiriki zoezi la kutengeneza chaki katika kiwanda cha
Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Wilaya ya
Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amebeba ili kuzianika chaki alizotengeneza
Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri
ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha kutengeneza jasi cha Dober Color
Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote Mkoani Singida kuagiza
chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.
Dkt Nchimbi ametoa
katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda viwili vinavyozalisha
chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa
kwa wingi na ikiwa haijapata soko.
“Hawa wenye viwanda
wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa kwa bei sahihi lakini
shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni karibu wanaagiza Dar es salaam
na mikoa mingine”, amesema na kuongeza kuwa,
“Yani mnasubiri chaki
hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka huko, hii haikubaliki,
kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa ili tupunguze gharama pamoja na
kuinua viwanda vyetu”.
Dkt Nchimbi ameongeza
kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika Viwanda vya Singida,
vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa kuunga mkono viwanda hivyo.
Amezitaka halmashauri
kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa viwanda hivyo hasa kwa
kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda katika machimbo ya jasi yanayotumika
kutengeneza chaki kwakuwa wenye viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa
barabara hizo.
Aidha Dkt Nchimbi
ametoa wito kwa wenye viwanda wote nchini ambao wanatumia madini ya jasi (gypsum)
katika shughuli zao wasihangaike kutafuta madini hayo bali waje singida kuna
viwanda vinatengeneza madini hayo kwa ubora mzuri na bei nzuri.
Amesema viwanda vya
kutengeneza jasi Singida vimekuwa vikizalisha madini hayo kwa wingi hivyo wenye
uhitaji wa madini hayo kutengenezea chaki, gypusum board POP, wanakaribishwa
kununua madini hayo mkoani hapa.
Dkt Nchimbi
amewapongeza wenye viwanda hivyo kwa kutumia rasilimali kama madini ya jasi
iliyopo Singida kwa kuanzisha viwanda mabavyo vinatengeneza ajira na kukuza
uchumi kwa kuwa wao wamekuwa walipa kodi wazuri.
Naye Meneja wa
kiwanda cha chaki cha Dober Color kilichopo Itigi Abdul Mahamoud amemshukuru Mkuu
wa Mkoa kwa hatua yake ya kukataza kuagizwa chaki nje ya Singida kwakuwa
kutaongeza soko ambalo litasaidia viwanda hivyo kukua.
“Mkuu wa Mkoa
tunashukuru kwa katazo hilo kwakuwa litafanya viwanda vyetu vikue na kuongeza
uzalishaji, lakini pia itafanya viwanda hivi viongeze ajira na hata kodi tunayolipa
itaongezeka hivyo kukuza uchumi wa Singida”, amesema Mahamoud.
Wafanyakazi wa
kiwanda cha Dober Color wakifungasha chaki, Meneja wa Kiwanda hicho amesema sehemu
ya kufungasha chaki hiyo inafanywa na wanawake
kwakuwa wako makini na haraka.
Mkuu wa Mkoa Singida
Dkt Rehema Nchimbi akikagua ubora wa chaki inayozalishwa katika kiwanda cha
Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, kushoto kwake ni Meneja
wa Kiwanda hicho Abdul Razak Mahamoud.
No comments:
Post a Comment