Mkurugenzi Bravo Kizito Lyampembile (wa kwanza kushoto) na Meya
Manispaa ya Singida, Chima Gwae (katikati) wakitiliana saini mkataba wa mradi
mkubwa wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 5.75 za mjini hapa kwa
kiwango cha lami,na mwakilishi wa kampuni ya China Henan Internatioanl Co
operation Ltd ya jijini Dar es salaam, Bi. Zephyr Liu. Ujenzi huo utagharimu
zaidi ya shilingi 13.1 bilioni ambazo zimetolewa na benki ya dunia.
Halmashauri
ya manispaa ya Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 13.1 bilioni, kwa
ajili ya kugharamia miradi mitatu ya uimarishaji miji (ULGSP) inayogharamia na
benki ya dunia.
Hayo
yamesemwa juzi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida Bravo Kizito
Lyapembile, wakati akizungumzia kwenye hafla ya sherehe ya kusaini mkataba
baina ya manispaa, washauri na mkandarasi atakayetekeleza miradi hiyo.
Amesema
wamefikia hatua hiyo ya kusaini mkataba baada ya taratibu zote za kisheria za
manunuzi kukamilika na kuongeza kuwa miradi hiyo ni ya ujenzi wa barabara zenye
urefu wa kilometa 5.75 kwa kiwango cha lami.
“Barabara
hizo ni pamoja na ile inayoanzia kituo cha mafuta Namfua hadi ofisi ya Mamlaka
ya mapato (TRA) ambayo itapanuliwa na kuwa mbili (double road). Nyingine ni ile
inayoanzia ofisi za TRA hadi makazi ya askofu wa kanisa la katoliki (barabara
ya Kinyeto)”, ameongeza.
Lyampembile
amesema taratibu za manunuzi katika mkataba huu zilianza mwezi Mei mwaka jana
na kukamilika Januari mwaka huu ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi ya shilingi
12.4 bilioni.
“Leo
hii manispaa ya Singida itatiliana saini mkataba namba LGA/115/SMC/2016/2017
/W/NO.1 na kampuni ya China Henan International Co-operation Group Co.LTD (CHICO)
ya jijini Dar-es-salaam. Ujenzi huo utakamilika baada ya miezi 12”, alifafanua
zaidi.
Amesema
CHICO atasimamiwa na kampuni ya Luptan Consultants Ltd ya jijini
Dar-es-salaam kwa gharama ya shilingi 648.3 milioni na itakamilika baada ya
miezi 15. Mkataba wa mradi huo ni LGA/115/SWMC/2016/2017/C/No.02.
“Vile
vile tutatekeleza mradi mwingine wa uandaaji wa mpango mkakati wa miaka mitano
wa mansipaa yetu ya Singida.Mradi huu wenye mkataba
LGA/115/SMC/2016/2017/C/No.03 una thamani ya zaidi ya shilingi 55.9
milioni.Mradi huu utatekelezwa na mshauri mwelekezi chuo cha mipango Dodoma,
Titus Mwageni”,alisema.
Sherehe
hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo,zilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Singida
Elias Tarimo na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi.
Dk.Nchimbi
Alitumia fursa hiyo kuyaomba mashirika ya TANESCO,TTCL na mamlaka ya maji
(SUWASA) kutoa ushirikiano na mkandarasi,ili miundo mbinu yao isikwamishe
utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utakapokamilika,utabadilisha madhari ya
mji wa Singida.
No comments:
Post a Comment