Vijana 43 wa
kihadzabe wakipunga mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya JKT Makutopora
kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya
kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha
maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw.
Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya utawala na
rasilimali watu akiwaaga Vijana 43 wanaojiunga na kambi ya JKT Makutopora
kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema
wakiwa jeshini watafundishwa uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu,
amewaasa wazazi kuwapeleka shule wanafunzi na kupokea fursa kama za jeshi.
Afisa Tawala ofisi ya Mshauri wa Mgambo
Rhinocerus Magembesoni akiwaasa vijana 43 wa kihadzabe wakipanda mabasi
kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi
hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na
mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao
kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
Vijana 43 wa
kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha
KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara
baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe
huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali
na mizizi.
Mmoja wa kijana wa kihadzabe
Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake wanawinda
na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze kuisaidia familia
yake lakini pia aweze kulitumikia taifa.
Vijana wa kihadzabe ambao
walikuwa wanawinda na kurina asali, wamesema wameamua kujiunga na jeshi ili waweze
kusaidia familia yake lakini pia waweze kulitumikia taifa.
No comments:
Post a Comment