Gari la Mkuu wa Mkoa wa
Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe likisukumwa na wananchi wa
kijiji cha Sagara baada ya kushusha neema kwa wakazi hao kwa kitendo cha
kuwamilikisha shamba la ekari 5,430. Wananchi hao kwa miaka mingi wamekuwa
wakitozwa shilingi elfu 30 kwa ekari moja katika msimu wa kilimo. Ushuru huo
kwa msimu huu ulipandishwa hadi shilingi 40,000 kwa ekari. Kwa sasa hawatalipa
tozo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kijiji cha Sagara na vijiji jirani juzi. Mheshimiwa
Mhandisi Mtigumwe ameagiza wakazi wa kijiji cha Sagara watumie shamba linalomilikiwa
na halmashauri ya Singida bila kubughuziwa wakati anaendelea na taratibu ya
kufuta umiliki wa shamba hilo na halamshauri ya wilaya ya Singida.
Mbunge wa jimbo la Singida
kaskazini Mhe. Lazaro Samwel Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na umati mkubwa wa kijiji cha Sagara kata ya Ngimu. Pamoja na
mambo mengine Mhe Nyalandu aliiomba serikali ingalie uwezekano wa kuwakabidhi
wananchi wa kijiji cha Sagara shamba lenye ukubwa wa ekari 5,430 ambalo halmashauri
ya wilaya ya Singida imeshindwa kuliendeleza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Singida Mheshimiwa Martha Mlata (wa pili kushoto) pamoja na mbunge wa jimbo la
Singida kaskazini Mheshimiwa Lazaro Samwel Nyalandu wakijumuika na kikundi cha
uhamasishaji cha kijiji cha Sagara kuburudisha wananchi waliohudhuria mkutano
wa hadhara juzi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa na
mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata akitoa nasaha zake kwenye
mkutano wa hadhara kijiji cha Sagara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Singida
Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe ili aweze kuongea na wananchi hao.
Mlata ameahidi chama cha CCM kitasimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ili iweze kutekelezwa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment