Wednesday, May 18, 2016

TUNAJALI WATOA KOMPYUTA 21 SINGIDA

Programu ya Tunajali imetoa kompyuta 21 zenye thamani ya shilingi milioni 60 kwa Mkoa wa Singida kwa ajili ya kusaidia shughuli za mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.

Akipokea kompyuta hizo Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina M. Lutambi amesema msaada huo utatumika ipasavyo katika kutasaidia ufuatiliaji na utathmini wa vituo vya huduma na tiba vya VVU. 

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina M. Lutambi akipokea kompyuta hizo kutoka kwa Meneja wa  programu ya TUNAJALI Mkoa wa Singida Christopher Hamaro.

Dokta Lutambi amewaagiza wasimamizi wa vituo vitakavyopatiwa kompyuta hizo wazitumie katika ufuatiliaji na tathmini, kuagiza dawa katika duka la dawa la serikali (MSD), kurekodi kumbukumbu za Bima ya Afya ya Mfuko wa jamii (CHF) na kufuatilia watoto waliozaliwa na akina mama wenye virusi vya Ukimwi.

Ameishukuru TUNAJALI kwa msaada huo na kwa ufadhili wa vipimo na dawa za kupunguza makali ya VVU, huduma za saratani ya shingo ya kizazi na huduma za watu waishio na VVU kwa ngazi ya Kaya kupitia vikundi vya asasi za  SEMA, Iambi, Faraja, Mt. Gasper na Hospitali ya Makiungu.

Naye Meneja wa Programu ya TUNAJALI Mkoa wa Singida Christopher Hamaro amesema wametoa kompyuta 187 zenye thamani ya shilingi milioni 523.8 kwa mikoa ya Njombe, Iringa , Morogoro, Dodoma na Singida.

Hamaro amesema Mkoani Singida kompyuta hizo ni kwa ajili ya Halmashauri za Wilaya za Mkalama, Singida, Iramba, Ikungi na Manyoni na pia katika vituo vya Queens of Universe, Makiungu, Mt. Gasper, Iambi, Puma House, Sokoine na Kinyangiri.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Dokta Erick Bakuza akipokea kompyuta zilizotolewa na TUNAJALI kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina M. Lutambi.

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.

No comments:

Post a Comment