Tuesday, September 29, 2015

MAFUNZO YA WARATIBU, MAAFISA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MIKOA YA SINGIDA NA DODOMA YAANZA RASMI LEO MKOANI SINGIDA.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Parseko Vicent Kone akifungua mafunzo ya waratibu, maafisa na wasimamizi wa uchaguzi wa Mikoa ya Singida na Dodoma leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 
Hakimu Ticky James Yamungu amewaapisha viapo vya usiri na kujitoa vyama vyovyote vya siasa waratibu, maafisa na wasimamizi wa uchaguzi wa Mikoa ya Singida na Dodoma.
 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Joseph Mchina akila kiapo cha usiri wa kusimamia uchaguzi Mkuu katika Manispaa ya Singida.
 


Waratibu, maafisa na wasimamizi wa uchaguzi wa Mikoa ya Singida na Dodoma wakiapa viapo vya usiri na kujitoa kwenye vyama vya siasa kabla ya kuanza kupata mafunzo juu ya uchaguzi.
 

Kaimu Mkuu Afisa Kanda wa kanda ya kati kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Martina J. Magaulla akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za viapo kwa waratibu, wasimamizi na maafisa wa uchaguzi kutoka mikoa ya Dodoma na Singida.


No comments:

Post a Comment