Tuesday, May 26, 2015

MASHINDANO YA UMISSETA MKOA WA SINGIDA YAANZA RASMI LEO.Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba akirusha tufe kama ishara ya ufunguzi wa mashindano ya Umisseta Mkoa wa Singida yanayofanyika  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mwenge mapema leo asubuhi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba ameziagiza kamati za michezo ya Umisseta Mkoa wa Singida kutumia weledi wa hali ya juu na umakini katika kuchagua timu zitakazowakilisha mkoa katika mashindano hayo kwa ngazi ya kanda.
 
Mumba ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mwenge wakati akizindua rasmi mashindano ya Umisseta ngazi ya Mkoa.
 
Ameongeza kuwa mashindano ya umisseta ni chachu ya kuwafanya vijana kuwa na afya bora, kupata ajira, kujenga ushirikiano baina yao na uzalendo.
 
 
 
 
 
Afisa Mchezo Mkoa wa Singida Henry Kapella akisoma taarifa kuhusu mashindao ya Umisseta ngazi ya Mkoa.

Naye Afisa Mchezo Mkoa wa Singida Henry Kapella amesema mashindano hayo yana jumla ya wana michezo 601 kutoka halmashauri sita za mkoa wa Singida ambao wataunda timu za Mkoa.
 
Amesema kuwa mashindano hayo yataunda timu mbalimbali za michezo ya bao, Sanaa za maonesho, riadha, mpira wa pete, wa miguu, wa mikono, wa kikapu, wa meza na wa wavu.
 
 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida Aziza Mumba akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo kutoka shule za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Singida katika mashindano ya Umisseta Mkoa wa Singida yanayofanyika  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mwenge mapema leo asubuhi.
Wanamichezo kutoka shule za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Singida wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Singida katika mashindano ya Umisseta Mkoa wa Singida yanayofanyika  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mwenge mapema leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment