Saturday, April 25, 2015

WIKI YA CHANJO YAZINDULIWA MKOANI SINGIDA; MKUU WA MKOA ASISITIZA UMUHIMU WA CHANJO.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akitoa matone ya vitamini A kwa mmoja watoto, wakati akizindua wiki ya chanjo Mkoani Singida, iliyofanyika tarafa ya Iguguno wilayani Mkalama.

Akina mama wakiwa na watoto wao wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida, uliofanyika tarafa ya Iguguno wilayani Mkalama.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Parseko V. Kone akizungumza na wakazi wa tarafa ya Iguguno waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida, uliyofanyika tarafa ya Iguguno wilayani Mkalama.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkalama James Mpinga akitoa ushuhuda wa umuhimu chanjo kwakuwa alipata matatizo ya ulemavu kwa kukosa chanjo wakati akiwa mtoto. Mpinga amewasihi wakazi wa Iguguno na Mkoa wa Singida kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hasa katika wiki hii ya chanjo.

Nesi akimchoma mtoto sindano ya chanjo ya surua wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida uliofanyika tarafa yya Iguguno Wilayani Mkalama.

No comments:

Post a Comment