Monday, September 08, 2014

WARSHA YA MREJESHO KWA WADAU WA MATOKEO YA TAFITI ZA MKUHUMI NA MABADILIKO YA TABIA NCHI YAFANYIKA MKOANI SINGIDA.

Washiriki wa warsha ya Mkuhumi Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa warsha hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.

Miradi ya Mpango wa Kupunguza uzalishaji wa Hewa ukaa (MKUHUMI) inayotokana na ukataji miti itafanikiwa kwa kiwango kikubwa endapo wananchi watahamasishwa na kuona faida za moja kwa moja za miradi hiyo.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan ametoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati akifungua warsha ya mrejesho kwa wadau wa matokeo ya tafiti za Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi zilizofanyika katika vijiji vitano  vya Mkoa wa Singida.
 
Hassan amesema  lengo la Mkuhumi ni kuiondosha  hewa ukaa katika anga na kuhifadhi katika misitu, pia kuziwezesha jamii zinazoishi katika maeneo ya misitu kunufaika na faida za nyingine za mpango huo kama vile kujipatia mapato yanayotokana na kuuza hewa ukaa iliyohifadhiwa.
 
Ameongeza kuwa  mapato yanayotokana na kuuza hewa ukaa yangehamasisha jamii kusimamia misitu na mazingira na hivyo kuongeza utunzaji  wa mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.
 
Aidha utafiti wa Mkuhumi umefanyika pia katika msitu wa mgori ulioko Halmashauri ya Singida Vijijini, ukilenga kuangalia mabadiliko ya tabia nchi katika msitu huo na mbinu zipi bora zimekuwa zikitumika katika kuhifadhi msitu huo.  Mgeni rasmi wa warsha ya Mkuhumi Mkoani Singida Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.Wa kwanza kushoto ni Dokta Dos Santos Silayo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine  na anayefuata ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bw. Mwendahasara Maganga.Washiriki wa warsha ya Mkuhumi Mkoa wa Singida wakimsikiliza mgeni rasmi wa warsha hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan.

No comments:

Post a Comment